Waziri wa Nchi Uwekezaji Mhe.Soraga amesema Serikali inaendelea kuboresha vivutio vya uwekezaji.

Waziri wa Nchi Uwekezaji Mhe.Soraga amesema Serikali inaendelea kuboresha vivutio vya uwekezaji.

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kufanya jitihada mbali mbali katika kuboresha vivutio vya uwekezaji hapa nchini. Ameyasema hayo Afisi kwakwe Mwanakwerekwe wakati alipokutana na Kaimu Kamishna kutoka Ubalozi wa Uingereza Nchini Tanzani Bw. Rick Stern aliekuja kwa lengo la

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kufanya jitihada mbali mbali katika kuboresha vivutio vya uwekezaji hapa nchini.

Ameyasema hayo Afisi kwakwe Mwanakwerekwe wakati alipokutana na Kaimu Kamishna kutoka Ubalozi wa Uingereza Nchini Tanzani Bw. Rick Stern aliekuja kwa lengo la kuelezea kuhusu mkutano wa majadiliano ya Kiserikali baina ya Serikali ya Tanzania na Uingereza katika kongamano la biashara la uwekezaji, usimamizi wa kodi pamoja na utaratibu wa kutunga sera na sheria, litakalofanyika tarehe 16 Novemba mwaka huu katika ukumbi wa J.N.I.C.C Jijini Dar- es- salaam.

Waziri Soraga amesema kupitia mkutano huo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inamatumaini makubwa ya kujadili na kuangalia namna gani nchi hizi mbili zinashirikiana katika mambo mbali mbali, na kusema kuwa Zanzibar inatumia teknolojia ya mtandao katika kutangaza vivutio vya uwekezaji.

Kwa upande wake Kaimu Kamishna kutoka Ubalozi wa Uingereza Nchini Tanzani Bw. Rick Stern amesema mkutano huo utajumuisha mijadala mbali mbali itakayostawisha mashirikiano baina ya Tanzania na Uigereza.

Katika mkutano huo Serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar itawakilishwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim Ali ambao wataelezea hatua za Serikali ya Mapiduzi ya Zanzibar zinazochukuliwa kuimarisha mazingira ya uwekezaji pamoja na kuelezea mikakati ya utekelezaji wa sera ya uchumi wa buluu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »