TIGO WASHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA ZA KIFEDHA

TIGO WASHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA ZA KIFEDHA

Na Mwandishi Wetu. Mtandao Namba moja unaoongoza kwa Utoaji wa Huduma za Kidigitali hapa nchini Tigo Tanzania , umeshiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kifedha yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar Es Salaam na kauli mbiu kwa Mwaka huu ni “Boresha Maisha kupitia Elimu ya Fedha” Maadhimisho haya yameandaliwa na Wizara

Na Mwandishi Wetu.

Mtandao Namba moja unaoongoza kwa Utoaji wa Huduma za Kidigitali hapa nchini Tigo Tanzania , umeshiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kifedha yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar Es Salaam na kauli mbiu kwa Mwaka huu ni “Boresha Maisha kupitia Elimu ya Fedha”

Maadhimisho haya yameandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango na walengwa wakuu katika Maonesho hayo ni asasi mbalimbali za kiraia na Watoa Huduma za kifedha kama vile TIGO PESA.

Akizungumza katika Maadhimisho hayo Meneja wa Huduma za Malipo TIGO PESA Bwana Reuben Kamuga amewakaribisha Wateja wa Tigo na Watanzania kwa Ujumla kutembelea Banda la Tigo lililopo katika Maadhimisho hayo kwa ajili ya kujionea Bidhaa mbalimbali walizonazo pamoja na kupewa elimu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana hasa na Huduma za Kifedha.

“Kutoka Tigo Pesa tuna Bidhaa nyingi kama ambavyo mnafahamu kwamba tunatoa huduma nyingi za kifedha lakini pia ni mda adhimu kabisa kuweza kuwakumbusha na kuwakaribisha wateja wetu katika ulimwengu wa Huduma zetu za Kidigitali mfano huduma kama Tigo Pesa Kibubu ambazo zinawawezesha wananchi na watumiaji wa Tigo Pesa kuendelea kuhifadhi fedha zao kwa irahisi na usalama pamoja na kupata gawio la asilimia kadhaa, kitu ambacho kinawawezesha kufikia malengo ya kibiashara na binafsi katika maisha yao ya kila siku , lakini pia tuna huduma kama vile LIPA KWA SIMU ambazo zinawasaidia wafanyabiashara wadogo kuanzia Machinga kuweza kukusanya malipo yao kutoka kwa wateja wao nchini , na hatujalenga katika utoaji wa huduma tu bali pia tunatoa elimu kwa wateja wetu wa TIGO PESA kuhusu namna ambavyo huduma zetu zinaweza zikasaidia kurahisisha na kuboresha maisha yao katika matumizi yao ya kila siku kwa sababu sisi tunaamini katika serikali na imesema kwamba uchumi unakua na ndio maana sisi tunaendelea kurahisisha zaidi namna ambavyo wateja wetu wanafanya miamala yao kitu ambacho kitaendelea kusaidia katika ukuaji wa uchumi wao”. Alimalizia Bwana Reuben

Kwa huduma mbalimbali zinazohusu Tigo Pesa Tafadhari Tembelea maduka ya TIGO yaliyoko nchi nzima.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »