TIGO NA WAKANDI KULETA NEEMA KWA SACCOS

TIGO NA WAKANDI KULETA NEEMA KWA SACCOS

Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za Kidigitali nchini Tigo Tanzania imetia saini ya Makubaliano na Kampuni ya Norway inayofahamika kwa jina la Wakandi Group AS, ili kurahisisha huduma za kifedha kidigitali kwa kupitia Tigo Pesa kwa SACCOS na taasisi ndogondogo za kifedha zilizosajiliwaTigo pesa imeunganisha jukwaa lake la malipo na Wakandi’s Credit Association Management

Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za Kidigitali nchini Tigo Tanzania imetia saini ya Makubaliano na Kampuni ya Norway inayofahamika kwa jina la Wakandi Group AS, ili kurahisisha huduma za kifedha kidigitali kwa kupitia Tigo Pesa kwa SACCOS na taasisi ndogondogo za kifedha zilizosajiliwa
Tigo pesa imeunganisha jukwaa lake la malipo na Wakandi’s Credit Association Management System ( CAMS) Kwa ajili ya SACCOS na taasisi ndogo za fedha ili kudhibiti huduma zao za kifedha kwa ufanisi na Kidigitali kwa urahisi na usalama zaidi.

Akizungumza katika tukio hilo Afisa Mkuu wa huduma za Kifedha Tigo Pesa Bi. Angelica Pesha alisema

“SACCOS sasa zimekomaa zaidi na zinahitaji jukwaa la kisasa la usimamizi wa fedha hii ni kutokana na sababu kuwa wanahifadhi kiasi kikubwa cha fedha , wanatoa mikopo na kusimamia riba zake, na ndio maana sisi kama Tigo Pesa tukachukua fursa hiyo kwa kushirikiana na Wakandi kuweka miamala yote ya SACCOS katika Mfumo wa Kidigitali kote nchini .

“Wakandi ina idadi kubwa ya wateja katika eneo lote la Afrika Mashariki kwahiyo ushirikiano huu unatupatia faida ya kiushindani kuwafikia wote waliotengwa katika huduma hizi za fedha za Kidigitali hasa katika SACCOS, kupitia mfumo huu wanachama wataweza kutumia akaunti zao za Tigo pesa kuchangia amana zao za SACCOS na kurejesha mikopo kupitia katika mfumo huohuo.
Alimalizia Bi. Pesha.

Kwa upande mwingine Mkurugenzi Mkuu wa Wakandi Bwana Espen Kvelland amesema kuwa“SACCOS sasa zimekomaa zaidi, na zinahitaji jukwaa la kisasa zaidi la usimamizi wa fedha. Wanahifadhi kiasi kikubwa katika akiba, kutoa mikopo, na kusimamia maslahi. Kwa hiyo, hii ni fursa kwa Tigo Pesa kushirikiana na Wakandi kuweka miamala yote ya SACCOS katika mfumo wa kidijitali kote nchini.”
“Wakandi ina idadi kubwa ya wateja katika eneo lote la Afrika Mashariki kwa hiyo ushirikiano huu unatupatia faida ya kiushindani kufikia watu waliotengwa kifedha nchini Tanzania na hasa katika nafasi za SACCOS. Wanachama wanaweza kutumia pochi zao za Tigo Pesa kuchangia amana zao za SACCOS na kurejesha mikopo kupitia chaneli hiyo hiyo, Tigo Pesa, Pesha ilisema.
“Sisi, Wakandi, tunalenga kufikia viwango vipya zaidi kwa kutumia Tigo Pesa na kusaidia SACCOS kuingia katika mfumo wa kidigitali wa kifedha. Ni fursa kwetu kujiimarisha zaidi katika soko la Tanzania. Ushirikiano huu ni hatua muhimu katika safari yetu ya kutoa uzoefu usio na pesa barani Afrika.

Ili kupata huduma hiyo, SACCOS na Taasisi Ndogo za Kifedha zinahitaji kusajiliwa na Wakandi Credit Association Management System (CAMS) kwa ajili ya wanachama wao, ambao ni wateja wa Tigo Pesa ili kukamilisha miamala yao bila matatizo kupitia menyu ya Tigo Pesa 15001# au kupitia Tigo Pesa App. .

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »