RAIS DK.MWINYI AMEFUNGUA JENGO LA WAGONJWA WA AKILI KIDONGOCHEKUNDU

RAIS DK.MWINYI AMEFUNGUA JENGO LA WAGONJWA WA AKILI KIDONGOCHEKUNDU

                               STATE HOUSE ZANZIBAR                        OFFICE OF THE PRESS SECRETARY                                           PRESS RELEASE Zanzibar                                                                        Novemba 18, 2021 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameitaka Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na watoto pamoja na Tume ya Uratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbali

                               STATE HOUSE ZANZIBAR

                       OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

                                          PRESS RELEASE

Zanzibar                                                                        Novemba 18, 2021

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameitaka Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na watoto pamoja na Tume ya Uratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbali mbali zinazohusu mfumo wa utoaji wa huduma za ‘Methodone’ kwa watu walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya.

Dk. Mwinyi ametoa agizo hilo katika Viwanja vya Hospitali ya Wagonjwa wa Akili Kidongochekundu Jijjini hapa, katika hafla ya ufunguzi wa Jengo la Hospitali ya wagonjwa wa akili, lililojengwa kwa mashirkiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wafadhili kutoka nchini Norway.

Amesema ana taarifa za kuwepo usimamizi usioridhisha katika utoaji wa huduma hizo, akibainisha kuwepo kasoro kubwa katika ufuatiliaji wa maendeleo ya tabia za wanaowapa huduma.

‘Tusifike mahala kitengo hiki cha kutoa huduma za methadone kikageuzwa ‘kijiwe’ cha kuyakutanisha makundi mbali mbali ya wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya’, alisema.

Dk. Mwinyi alisema  ana taarifa za kuwepo manung’uniko kutoka kwa wakaazi wa eneo hilo la Kidongochekundu na maeneo jirani juu ya ongezeko la uhalifu unaofanywa na baadhi ya wathirka wanaofika hapo kufuata tiba.

Aliuagiza uongozi wa Tume hiyo kuharakisha ujenzi wa Kituo cha Kurekebisha Tabia kwa waathirika wa Dawa za kulevya  unaoendelea katika eneo al Kidimni Wilaya Kati pamoja na kuagiza kuanza kwa ujenzi wa kituo kama hicho katika eneo la Kangagani Wilaya Wete Pemba.

Alisema ujenzi wa vituo hivyo utawezesha kuwatibu na kuwasaidia waathirika katika sehemu zizlizo faragha na bila kutishia usalama wa wananchi na mali zao.

Aidha, Dk. Mwinyi alisiistiza haja ya kuacha kuwanyanyapaa waathirika  na badala yake jamii ishirikiane nao na kuwasaidia,.

Katika hatua nyengine, Rais Dk, Mwinyi aliuagiza Uongozi wa Wizara Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto kuharakisha utekelelzaji wa mipango itakayowezesha upatikanaji wa wafanyakazi na  vifaa tiba ili jengo lililofunguliwa liweze kutoa huduma kwa kiwango kilichokusudiwa.

 Alisema magonjwa ya akili ni changamoto kubwa kwa nchi zote duniani, akibainisha takwimu za Shirika la Afya Duniani zinazoeleza kuwa kila penye watu wanne, kuna mtu mmoja mwenye uwezekano wa kupata ugonjwa huo maishani mwake.

Alisema kutokan na kiwango hicho kikubwa, kuna umuhimu wa kuwepo mipango na mikakati mahsusi ya kupunguza kasi ya ugonjwa huo na kuwasaiadia waathirika.

Alisiiitiza umuhimu wa jamii kuhakikisha inaimarisha utamaduni wa kupendana, kusaidiana, kuliwazana na kufarijian wakati wa shida na misukusuko, sambamba na kujumuika pamoja ili kupunguza msongo wa mawazo.

Aidha alikumbusha umuhimu wa jamii kuimarisha malezi ya watoto, sambamba na kutaka nguvu kubwa kutumika katika mapambano dhidi ya uingizwaji na matumizi ya dawa za kulevya.

Mapema, Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto Nassor Ahmeid Mazrui alisema Wizara hiyo inaendelea na juhudi za kuhakikisha afya za wananchi wa Zanzibar zinaimarika na kuwa bora.

Alisema katika kipijndi kifupi kijacho Wizara hiyo itaipatia vifaa vya uchunguzi hospitali hiyo  ili kuwaondolea usumbufu wagonjwa wanaofika kufuata tiba, huku lengo likiwa ni kuondoa changamoto zote zinazoikabili sekta ya afya.

Nae, Mfadhili wa Ujenzi huo Trond Mond alisema kwa kipindi kirefu sasa Chuo Kikuu cha Hackland kutoka nchini Norway kimekuwa  na urafiki na ushirikiano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na hivyo kupata fursa ya kuwakilisha misaada mbali mbali katika sekta ya Afya.

Alisema miongoni mwa misaada hiyo ambapo Hospitali ya wagonjwa wa Akili  Kidongochekundu imekuwa ikipokea ni pamoja na miundombinu, kuwajengea uwezo watendaji pamoja na vifaa mbali mbali.

Kitengo cha habari,

Ikulu Zanzibar

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »