App mpya ya Kiswahili kuwezesha watoaji huduma za uzazi salama {+Video}

App mpya ya Kiswahili kuwezesha watoaji huduma za uzazi salama {+Video}

Taasisi ya Afya Ifakara kwa kushirikiana na Maternity Foundation na Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania pamoja na Ole Kirk Foundation leo hii inazindua toleo la Kiswahili la “Safe Delivery App” – nyenzo ya mafunzo kwa njia ya simu na msaada kwa watoa huduma za afya ili kuhakikisha uzazi salama kwa akina mama na watoto wachanga

Taasisi ya Afya Ifakara kwa kushirikiana na Maternity Foundation na Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania pamoja na Ole Kirk Foundation leo hii inazindua toleo la Kiswahili la “Safe Delivery App” – nyenzo ya mafunzo kwa njia ya simu na msaada kwa watoa huduma za afya ili kuhakikisha uzazi salama kwa akina mama na watoto wachanga nchini Tanzania.

Wakunga nchini Tanzania wana shughulikia maisha ya akina mama na watoto wachanga mikononi mwao kila siku. Ili kuwasaidia katika kazi zao za kila siku – na katika mafunzo yao endelevu – Taasisi ya Afya Ifakara na Maternity Foundation wanatambulisha toleo la lugha ya Kiswahili la Safe Delivery App, nyenzo ya mafunzo kwa njia ya simu ili kudhibiti shida mbalimbali zinazohusiana na uzazi.

VIDEO: NAMNA YA KUTUMIA APP MPYA KUWEZESHA UZAZI SALAMA, KUZUIA VIFO VYA AKINA MAMA NA WATOTO

Licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na serikali, mashirika ya kiraia na mashirika ya kimataifa katika kuboresha upatikanaji wa huduma bora kwa akina mama na watoto wachanga nchini Tanzania, bado kiwango cha vifo vya uzazi ni 556 kwa kila watoto 100,000 kulingana na takwimu za mwaka 2016.

Moja ya ufumbuzi wa kuboresha afya ya uzazi ni kuongeza mafunzo yanayofaa na usaidizi kwa wahudumu wa afya, Safe Delivery App ni nyenzo inayofaa, bora na yenye ubunifu kufanya hivyo.

Application hii ni bure na inafanya kazi bila kuihitaji mtandao ukishaipakua, na hutumia maelekezo rahisi kuwaongoza wahudumu wa afya katika huduma za dharura za uzazi na watoto wachanga pamoja na matibabu ya Uviko-19 kwa kina mama wajawazito na watoto. Inajumuisha video, maswali ya majaribio, maelezo ya kufanya taratibu mbalimbali za kimatibabu, na orodha za dawa ambazo wakunga na wahudumu wa afya wanaweza kurejelea kila wakati – wakiwa kazini, ama katika muda wao wa ziada au kama sehemu ya mafunzo yao.

Kwa msaada wa Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania na Ole Kirk Foundation, Maternity Foundation na Taasisi ya Afya ya Ifakara wamekuwa wakishirikiana kutengeneza toleo la Kiswahili la Safe Delivery App tangu 2017, wakifanya kazi hii kwa karibu na wadau wakuu nchini ili kuhakikisha ubora wa maudhui na miongozo ya kimatibabu.

Kazi hiyo iliongozwa na Taasisi ya Afya Ifakara na washirika muhimu wakiwemo Chama cha Madaktari wa Watoto Tanzania (PAT) na Chama cha Madaktari wa Wanawake na Madaktari wa Uzazi (AGOTA) wakichangia katika uhakiki wa kina na urekebishaji wa maudhui ya kimatibabu kwenye App.

Utekelezaji wa App hii ya Kiswahili nchini kote utaanza baada ya kuzinduliwa Novemba 2021, ukiongozwa na Taasisi ya Afya Ifakara kwa ushirikiano wa karibu na Wizara ya Afya na mamlaka za afya za mikoa pamoja na Maternity Foundation.

Baadhi ya shughuli muhimu ni pamoja na mafunzo ya wahudumu wa afya na utambulisho wa App hii, pamoja na ufuatiliaji na tathmini ili kurekodi matokeo ya mafunzo haya na kuvumbua mbinu nyingine bora zaidi. Yote haya ili kuhakikisha msaada bora zaidi kwa wafanyakazi wa afya wanaotumia Application hii.“Tuna furaha kubwa sasa kuweza kuipeleka Apllication hii mikononi mwa wakunga na watoa huduma wa afya kote nchini Tanzania.

Wanaokoa maisha kila siku, na kwa nyongeza hii mpya kwenye kazi na mafunzo yao, tunaweza kuwaunga mkono katika hayo – shukrani kwa ushirikiano mkubwa uliokowepo katika kufanikisha hatua hii,” anasema Anna Felsen, Mkurugenzi Mtendaji wa Maternity Foundation.”Tuna matumaini kuhusu siku zijazo: Katika miaka ijayo, dhamira yetu inabakia kutambua mahitaji ya afya ya watu wetu na kuwaundia masuluhisho makubwa.

Kwa kutumia Safe Delivery App, wahudumu wetu wa afya sasa wana nyenzo mpya ya kujifunza kila wakati, kusasisha maarifa na ujuzi wao kuhusu jinsi ya kushughulikia matatizo mbalimbali yanayohusiana na ujauzito na uzazi, ili maisha yasipotee wakati wa kujifungua,” anasema Donat Shamba, Mratibu wa mradi nchini Tanzania.

Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mette Nørgaard Dissing-Spandet, pia ana furaha kwamba toleo la Kiswahili la Safe Delivery App hatimaye linazinduliwa: “Kuboresha afya ya uzazi na watoto wachanga ni kipaumbele cha Denmark na Tanzania.

Tukiwa na App hii, natumai tutaona kupungua kwa idadi ya akina mama wanaofariki wakati wakijifungua”.

Balozi wa Denmark pia ana shauku ya kuona kuwa Safe Delivery App inawekwa katika mfumo wa huduma za afya nchini ili kutoa matokeo endelevu.Safe Delivery App inapatikana kwenye Google Play na App store bila malipo.Kuhusu Taasisi ya Afya ya IfakaraTaasisi ya Afya Ifakara (Ifakara) ni shirika linaloongoza la utafiti barani Afrika lenye rekodi thabiti katika kuendeleza, kupima na kuthibitisha ubunifu kwenye afya.

Ikiendeshwa na jukumu kuu la kimkakati la utafiti, mafunzo na huduma, kazi ya Taasisi sasa inahusu wigo mpana, ikijumuisha sayansi ya matibabu na ikolojia, utafiti wa mifumo ya afya na tafsiri ya sera.

Kuhusu Maternity FoundationMaternity Foundation ni NGO ya Denmark inayofanya kazi kuboresha afya ya uzazi na watoto wachanga katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati.

Kwa kutumia masuluhisho ya kidijitali na mipango mikakati ya mafunzo, Maternity Foundation huwasaidia wakunga kushughulikia hatua za kuokoa maisha wakati wa ujauzito na kujifungua.

______________________MAWASILIANOKuhusu Mradi:#5 Mtaa wa Ifakara Kiwanja 463 Mikocheni | Kinondoni, Dar es Salaam +255 222 774 756 | +255 683 105 670 | dshamba@ihi.or.tzWanahabari –

Kwa Ajili ya Mahojiano:#5 Mtaa wa Ifakara Kiwanja 463 Mikocheni | Kinondoni, Dar es Salaam +255 222 774 756 | +255 629 155 157 | communications@ihi.or.tz

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »