VIONGOZI WASIOCHANJA WAJIUZULU-WAZIRI DKT. DOROTHY GWAJAIMA

VIONGOZI WASIOCHANJA WAJIUZULU-WAZIRI DKT. DOROTHY GWAJAIMA

Waziri wa Afya Dr. Dorothy Gwajima amesema msimamo wa Tanzania chanjo ni hiari bila malipo lakini kwa maoni yake yeye kama Kiongozi hajachanjwa na anaenda kuwaelimisha Wananchi anapaswa kujipima na kuachia ngazi “kwa maoni yangu Mimi hustahili, kaa pembeni na wewe uelimishwe na aliyeeelewa ukishaelewa ukawa wa mfano utarejea” “Wenye Mamlaka ya kuelimisha Watu wachanjwe

Waziri wa Afya Dr. Dorothy Gwajima amesema msimamo wa Tanzania chanjo ni hiari bila malipo lakini kwa maoni yake yeye kama Kiongozi hajachanjwa na anaenda kuwaelimisha Wananchi anapaswa kujipima na kuachia ngazi “kwa maoni yangu Mimi hustahili, kaa pembeni na wewe uelimishwe na aliyeeelewa ukishaelewa ukawa wa mfano utarejea”

“Wenye Mamlaka ya kuelimisha Watu wachanjwe na hawajachanjwa maana yake hawajaelimika, iwe aibu kwa Kiongozi uliyepewa dhamana ya kuwatumikia Wananchi na kuwaelimisha na wewe kuwa wa mfano halafu haujachanjwa, maana yake wewe huelewi na Wananchi wako hawaelewi, anatakiwa akae Mtu sahihi hapo anayeleewa na mwenye uwezo wa kuzungumza, anayefanya kwa vitendo”

“Viongozi ambao wanaelimisha Watu lakini wao hawajachanjwa itoshe tu kusema wanatakiwa wajipime kama wanatosha kuwaongoza Wananchi kwasababu wapo pale kwa dhamana ya Serikali na tunapoweka mipango na kusema tukaitekeleze tunatakiwa tuwe wa mfano, ndio maana Rais Samia aliongoza mapambano haya akaelimisha akachanja hadharani akifuatiwa na Viongozi wengine huu ndio Uongozi wenye mfano, sasa tunao Viongozi wababaishaji wasiochanjwa”

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »