RAIS DK. MWINYI AVITAKA VYUO VIKUU NCHINI KUANZISHA PROGRAMU MPYA KWA LENGO LA KUONGEZA FURSA ZA AJIRA

RAIS DK. MWINYI AVITAKA VYUO VIKUU NCHINI KUANZISHA PROGRAMU MPYA KWA LENGO LA KUONGEZA FURSA ZA AJIRA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amevihimiza vyuo vikuu na taasisi za Elimu Nchini kuendelea kuanzisha programu mpya ambazo ni muhimu katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Nchi ili kuongeza Fursa za ajira. Rais Dk. Mwinyi alieleza hayo kupitia hotouba iliosomwa kwa niaba yake na Makamu wa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amevihimiza vyuo vikuu na taasisi za Elimu Nchini kuendelea kuanzisha programu mpya ambazo ni muhimu katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Nchi ili kuongeza Fursa za ajira.

Rais Dk. Mwinyi alieleza hayo kupitia hotouba iliosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleima Abdulla katika sherehe za Mahafali ya 19 ya chuo kikuu cha Zanzibar University yaliofanya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

Alieleza kuwa vyuo vilivyopo nchini lazima vishike usukani katika kukuza ubunifu na viwe tayari kushiriki katika kubuni mipango muhimu ya maendeleo kwa taifa.

Dk. Mwinyi alionesha faraja yake kwa uongozi wa chuo hicho kwa kuanzisha programu mpya za masomo yanayohisiana na taaluma ya Afya katika ngazi ya uzamili na uzamivu.

Nae Mkuu wa Chuo kikuu cha (Zanzibar University) Mhandisi Dk. Abdulkadir Othman Hafiz aliipongeza serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirkiano wake katika kukiendeleza chuo hicho ambacho kimefanikiwa kutoa taalum kwa wananfunzi wengi nchini na ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla.

Kwa upande wake Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Haroonah Nsubuga alisema katika mahafali hayo ya 19 ya chuo hicho jumla ya wanafunzi 617 wamehitimu kupitia fani mbali mbali wakiwemo wanawake 345 na wanaume 272 kwa ngazi ya Astas-shahada, Stas-shahada, Shahada, Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Disemba 22, 2021.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »