Prof.Julian Murchison ameteuliwa kuwa Balozi wa utalii wa Tanzania Nchini Marekani .

Prof.Julian Murchison ameteuliwa kuwa Balozi wa utalii wa Tanzania Nchini Marekani .

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amemteua Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Michigan, Prof.Julian Murchison kuwa balozi wa hiari wa utalii wa Tanzania nchini Marekani ili kuongeza idadi ya watalii wanaotoka nchini Marekani   Hatua hiyo ni inakuja ikiwa ni jitihada za Wizara ya Maliasili na Utalii  kuanza kuteka soko endelevu la Utalii la Wanafunzi wa Vyuo

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Michigan, Prof.Julian Murchison ( wa kwanza kushoto) ambaye ameteuliwa  kuwa balozi wa hiari wa utalii wa Tanzania nchini Marekani akiwa kwenye picha ya pamoja na familia yake katika mji wa Detroit  mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake, Wa pili kulia ni Prof. Sandra Murchison ambaye ni mke wa Prof. Juliani na kwanza kulia ni Afisa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Jean Msabila
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Michigan, Prof.Julian Murchison ( wa kwanza kushoto) ambaye ameteuliwa  kuwa balozi wa hiari wa utalii wa Tanzania nchini Marekani  Wa kwanza kulia ni Prof. Sandra Murchison ambaye ni mke wa Prof. Juliani.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Michigan, Prof.Julian Murchison ( wa pili kushoto) ambaye ameteuliwa  kuwa balozi wa hiari wa utalii wa Tanzania nchini Marekani mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake ambaye kwa sasa anafakazi nyumbani kwake kutokana na uwepo wa UVIKO -19, Wa kwanza kushoto ni Prof. Sandra Murchison ambaye ni mke wa Prof. Julian na kwanza kulia ni Afisa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Jean Msabil

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amemteua Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Michigan, Prof.Julian Murchison kuwa balozi wa hiari wa utalii wa Tanzania nchini Marekani ili kuongeza idadi ya watalii wanaotoka nchini Marekani  

Hatua hiyo ni inakuja ikiwa ni jitihada za Wizara ya Maliasili na Utalii  kuanza kuteka soko endelevu la Utalii la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Marekani hususan vilivyopo katika Jimbo la Michigan 

Akizungumza hivi karibuni kwenye ziara ya kikazi katika mji wa Detroit nchini Marekani Waziri Ndumbaro amesema  amelazimika kumteua Balozi huyo kutokana na ushawishi wake mkubwa  katika jamii na pia Prof. Julian ni zao la Tanzania

Amesema  Prof. Juliani  amezaliwa nchini Marekani lakini amesoma na kuhitimu shahada yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na pia amekaa Tanzania kwa  zaidi ya  miaka 15

Aidha, Dkt. Ndumbaro amesema Prof. Julian mbali ya kuwa Mwenyeji nchini Tanzania bali ni mtu mahiri anayezungumza lugha ya kiswahili ya ufasaha wa hali ya juu.

Amesema anaamini  atakuwa  Balozi mzuri kwa utalii wa Tanzania kwa sababu maeneo mengi ya utalii anayajua hususani maeneo ya kusini ambako alitumia muda mwingi katika maeneo  hayo kufanya utafiti.

Aidha, Dkt. Ndumbaro amuelezea Prof. Juliani kuwa ni mtu mahiri anayezungumza Lugha ya Kiswahili kwa ufasha wa hali ya juu

“ Uteuzi wake sio wa kubahatisha ni mtu ambaye amekuwa anaipenda sana nchi ya  Tanzania ana amekuwa muumini mkubwa wa utalii wa utamaduni hivyo atakuwa chachu kwa Wanafunzi anaowafundisha kuwachochea kuja nchini Tanzania na hili ndo soko tunalolitaka kwa sasa” amesisitiza Dkt, Ndumbaro

Wizara ya Maliasili na Utalii imedhamiria kukuza utalii kwa kuongeza watalii kutoka Marekani kwa kuwa nchi hiyo ni ya pili kwa kuleta watalii wengi nchini  Tanzania

Kwa mujibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, takwimu za mwaka 2020/2021 zinaonyesha Marekani ilikuwa ya tano kwa idadi ya watalii  waliotembelea Tanzania huku Uingereza ikiwa ya 16.

Kwa upande wake, Prof. Julian amesema kuwa yeye atakuwa balozi mzuri katika kutangaza mazuri ya Tanzania na utalii wake duniani kote kwa wanafunzi anaowafundisha na pia kwa jamii yote inayomzunguka

“Kila nitakapopata fursa nitawaambia kuwa Tanzania ni nchi yenye watu wakarimu sana, nitazidi kuipeperusha bendera ya Tanzania na nitawaeleza sehemu mahsusi za kitalii zilizoko Tanzania.

Hata hivyo, Prof. Julian amesema hata kabla ya kuteuliwa amekuwa mstari wa mbele kutangaza vivutio vya utalii katika kazi yake anayoifanya ya kufundisha wanafunzi

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »