Serikali itaendelea kuajiri watumishi wa afya.

Serikali itaendelea kuajiri watumishi wa afya.

Serikali inaendelea kuboresha upatikanaji wa watumishi wa kada za Afya katika Vituo vya kutolea huduma za Afya ili kuendana na upanuzi wa miundombinu ya Afya ya Msingi nchini. Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Festo Dugange amesema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Nyangw’ale

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Festo Dugange.

Serikali inaendelea kuboresha upatikanaji wa watumishi wa kada za Afya katika Vituo vya kutolea huduma za Afya ili kuendana na upanuzi wa miundombinu ya Afya ya Msingi nchini.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Festo Dugange amesema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Nyangw’ale Mhe. Nassor Hussein Amar aliyetaka kujua serikali inampango gani wa kuongeza watumishi katika vituo vya afya vya Kharumwa na Nyangw’hwale.

Mhe. Dugange amesema katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Serikali iliajiri watumishi 2,726 wa kada mbalimbali za Afya katika ajira hizo za Serikali, Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale ilipangiwa watumishi 20 ambapo Kituo cha Afya Kharumwa kilipata watumishi 3 na Kituo cha Afya Nyang’hwale kilipata watumishi 4.

Aidha, amesema Serikali itaendelea kuajiri na kugawa watumishi kwenye Halmashauri na Vituo vya kutolea huduma za Afya kadiri ya upatikanaji wa vibali vya ajira na fedha ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »