WATENDAJI WA MTAKUWWA WATAKIWA KUBADILIKA

WATENDAJI WA MTAKUWWA WATAKIWA KUBADILIKA

Na WMJJWM, DodomaKatibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amewataka watendaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto (MTAKUWWA) kubadilika na kufanya kazi kwa matokeo.Dkt. Chaula ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Kamati tendaji inayojumuisha Idara na Wizara zinazotekeleza

Na WMJJWM, Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amewataka watendaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto (MTAKUWWA) kubadilika na kufanya kazi kwa matokeo.
Dkt. Chaula ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Kamati tendaji inayojumuisha Idara na Wizara zinazotekeleza Mpango huo.
Dkt. Chaula amesema kila mmoja anayehusika na kutekeleza Mpango huo atekeleze majukumu aliyopewa na matokeo yawe ya takwimu ili kiwe na uhalisia.
Amesema lazima kuwe na vigezo vya kuondoa changamoto za ukatili zilizopo ili matokeo yaonekane kuanzia ngazi ya vijiji na Mitaa.
“Utendaji wetu wa kazi uwe na matokeo, mpango huu wa miaka mitano kila mmoja atekeleze wajibu wake nakazi yoyote uliyopewa lazima iwe na matokeo kwa takwimu” alisema Dkt. Chaula
Ameongeza kuwa kama Kamati ikitekeleza majukumu yake, vitendo vya ukatili vitapungua na havitatokea katika jamii zetu.
Kwa upande wake Geoffrey Chambua mratibu wa mradi wa majaribio kutokomeza ukatili wa kingono amebainisha kuwa katika mradi huo uliofanyika kwa miezi mitatu Wilaya ya Kinondoni ilionekana kuna umuhimu wa kuwa na vituo vya mkono kwa mkono vinavyowasaidia waathirika wa ukatili wa kingono kupata huduma muhimu kwa pamoja na kwa wakati.
Naye Naibu Mkurugenzi wa shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo WILDAF Cesilia Assey, ameipongeza Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo kwa karibu na kutoa wito kwa wadau wote kushirikiana kutokomeza tatizo la ukatili.
Aidha amesema lengo ni kufikia hatua ya huduma kwa waathirika wa ukatili zinapatikana kwa urahisi na wananchi wanafikiwa kupata elimu kuhusu madhara ya ukatili katika Jamii.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »