Wakazi wa Buza Kanisani walalamikia Uchafuzi wa Mazingira wa Sauti

Wakazi wa Buza Kanisani walalamikia Uchafuzi wa Mazingira wa Sauti

Na Mwandishi Wetu Wakazi wa Buza Kanisani, Mtaa wa Amani, wamelamikia mfanyanya biashara kwa kujenga ukumbi wa sherehe katika eneo la makazi (residentional) , jambo linalosabisha uchafuzi mkubwa wa mazingira kwa njia ya sauti kutokana kelele zinatoka katika ukumbi huo. Wanamshutumu mfanyabiashara huyo Bw. Shayo kwa kuvunja sheria za matumizi ya ardhi kwa ukumbi wa

Na Mwandishi Wetu


Wakazi wa Buza Kanisani, Mtaa wa Amani, wamelamikia mfanyanya biashara kwa kujenga ukumbi wa sherehe katika eneo la makazi (residentional) , jambo linalosabisha uchafuzi mkubwa wa mazingira kwa njia ya sauti kutokana kelele zinatoka katika ukumbi huo.

Wanamshutumu mfanyabiashara huyo Bw. Shayo kwa kuvunja sheria za matumizi ya ardhi kwa ukumbi wa sherehe na bar kubwa kwenye la eneo ambalo limepimwa na mamlaka za Serikali kwa ajili ya makazi, na sio biashara.

“Tunashindwa kulala usiku, watoto wetu wanashindwa kujisomea usiku kwa kelele na ghasia zinasababishwa na ukumbi huu,” amesema bw.Mika Moza, mmoja wa wakazi wa eneo hilo.

“Serikali imetumia fedha nyingi za walipa kodi kupima maeneo haya ya makazi, iweje leo mtu anabadilisha matumizi ya ardhi kiholela kwa kufanya biashara kama hii yenye athari kubwa kwa mazingira kwa njia ya sauti/ kelele, alafu serikali ya mtaa iko kimya,” amesema mkazi mwingine, Kulwa Muga

Wakazi wamedai kuwa wamewasilisha malalamiko yao (kwa maandishi) kwa Afisa mipango miji- Manispaa ya Temeke tangu Mwaka 2013, lakini mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.

“Mfanyabiashara huyu Bw. Shayo, ni mbabe na kwa sababu ana pesa kiongozi wa serikali ya mtaa, maafisa wa mipango miji -Temeke Manispaa, wote wametiwa mfukoni, hawawezi kuthibiti jambo hili, hali inayosababisha hadha kubwa kwa wakaxi wa eneo hili,” Bi. Moza Mrope, amadai mkazi mwingine.

Kuthibisha mahusiana wenye mashaka kati mfanyabiashara huyo, wakazi wanasema baada ya kuvunja sheria kwa miaka za ya tisa, hivi karibuni maafisa mipango miji -Temeke manispaa wamemshauri Bw. Shayo, kubadilisha matumizi ya kiwanja hicho No. 686, Kitalu E, kutoka makazi kwenda biashara, jambo ambalo ni “uvunjifu wa sheria za mazingira.”

“Kumruhudu abadilishe matumizi ya kiwanja -kutoka makazi kwenda biashara, ni kosa kwa sababu maeneo haya yamepimwa kwa ajili makazi, na si biashara…Manispaa wakiruhusu jambo hili watakuwa wamebariki rasmi uchafuzi wa mazingira na uvunjaji wa sheri za mazingira, bila kujali athari za kelele na uchafu huu mkubwa wananchi walio wengi.

Alipohojiwa, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amani, Bw. Omary Katoto amesema “Sio wakazi wote wanalalamika kuhusu jambo hili, ninachofahamu mimi ni kwamba kulikuwa ugomvi kati ya mfanyabiashara huyo na mtu mmoja katika eneo hilo.”

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amani, Bw. Omary Katoto

“Miaka kama mitatu iliyopita walipelekana polisi, walitishiana maisha sijui, lakini niitwa kama Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa, nikawasihi polisi watuachie jambo lile tukalisuhishe kirafiki kama wa mtaa mmoja, walikubali …tulikaa chini tuongea na pande zote mbili, tukamaliza. Leo hii nashangaa kuone jambo hili nimeibuka tena.”.

Alipotafutwa, Afisa Ardhi-Temeke Manispaa, Salumu Ali, amesema “Njia rahisi kwa wakazi hao ni kupeleka malalamiko yao kwa maandishi kwa Mkurugenzi wa Manispaa, ili kuweka pingamizi la kuzuia mabadiliko ya matumizi ya Ardhi ambayo Bw. Shayo, amepanga kuyafanya—kutoka Makazi kwenda biashara.”

“Kama mamlaka, tutapokea maoni na mapingamizi ya wananchi hao, na kuyafanyia kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za maswala ya Ardhi. Hilo ndilo naona kama suluhisho kwa wakazi hao wanaolalamika.”

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »