UONGOZI WA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUHIMIZA UPANDAJI MITI

UONGOZI WA JIJI LA DODOMA WATAKIWA  KUHIMIZA UPANDAJI MITI

NAIBU Waziri wa Afya, Dokta Godwin Mollel amelitaka Jiji la Dodoma kuweka mkazo katika kuhamasisha wananchi kupanda miti badala ya kutoa maelekezo ya upakaji wa rangi kwenye mabati peke yake   huku akiwataka wananchi kuzingatia suala la usafi katika maeneo yao ili kuondokana na magonjwa ya kuambukiza yanayopelekea kutumia gharama kubwa kwa matibabu. NA FAUSTINE GIMU

NAIBU Waziri wa Afya, Dokta Godwin Mollel amelitaka Jiji la Dodoma kuweka mkazo katika kuhamasisha wananchi kupanda miti badala ya kutoa maelekezo ya upakaji wa rangi kwenye mabati peke yake   huku akiwataka wananchi kuzingatia suala la usafi katika maeneo yao ili kuondokana na magonjwa ya kuambukiza yanayopelekea kutumia gharama kubwa kwa matibabu.

NA FAUSTINE GIMU GALAFONI KUTOKA JIJINI DODOMA

INSERT..GIMU=MOLLEL

Dokta Mollel ametoa rai hiyo leo wakati akiongoza zoezi la usafi wa mazingira kwenye soko la Chang’ombe na kutoa elimu ya utenganishaji wa taka, mifuko na vifungashio vya plastiki ikiwa  ni sehemu ya wiki ya uzinduzi wa Sera Mpya ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021.

INSERT…1.MOLLEL

Pamoja na hayo, amehimiza wananchi kupata  chanjo ya UVIKO-19 ili kujikinga na maambukizo ya ugonjwa huo.

Naye, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mary Maganga amesema zoezi hilo lilianza Februari 7 mwaka huu ikiwa  ni muendelezo wa shughuli ya wiki ya uzinduzi wa Sera hiyo na inatarajiwa kuhitimishwa februari 12.

INSERT…2 MARRY

Kwa upande wake, Ofisa Mazingira wa Jiji hilo, Ally Mfinanga, amesema kuna umuhimu wa wananchi kutenganisha taka ikiwamo za plastiki ili kuipunguzia mzigo Halmashauri inayotumia asilimia kubwa ya fedha zake katika usafirishaji wa taka huku mwenyekiti wa soko la  Chang’ombe  Godfrey Mbilinyi akizungumzia walivyolipokea kuhusu elimu ya utunzaji wa mazingira.

INSERT……3 MFINANGA& MWENYEKEKITI SOKO 

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »