NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF )Tanzania Bara umetoa Msaada wa Vifaa Tiba ikiwemo Vitanda na Mashine kwa ajili ya kupima Shinikizo la damu kwa wagonjwa wanaopata matibabu katika Hospitali ya Mnazi mmoja iliyopo Visiwani Zanzibar ikiwa ni sehemu ya kuwajibika katika jamii. Katika kutoa msaada huo NSSF ilisindikizwa
NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF )Tanzania Bara umetoa Msaada wa Vifaa Tiba ikiwemo Vitanda na Mashine kwa ajili ya kupima Shinikizo la damu kwa wagonjwa wanaopata matibabu katika Hospitali ya Mnazi mmoja iliyopo Visiwani Zanzibar ikiwa ni sehemu ya kuwajibika katika jamii. Katika kutoa msaada huo NSSF ilisindikizwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kutoka na utendaji wa mashirikiano uliopo katika Mifuko hii.
Katika kuelekea Siku ya Wanamke Duniani Marchi 8 akizungumza leo na waandishi wa Habari, Meneja uhusiano na Elimu kwa Umma – NSSF Lulu Mengele kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF amesema Jukumu la kusaidia ni sehemu ya kuwajibika katika Jamii kwa kutoa misaada na kwa kutambua thamani ya mwanamke katika Jamii wameamua kutoa msaada wa vifaa tiba katika hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar. Wakati wa kutoa msaada huo NSSF imesindikzwa na ZSSF kwa lengo la kukuza mashirikiano baina ya Mifuko hii.
Naye Afisa utawala ZSSF Nassor Hassan katika tukio hilo ameishukuru uongozi wa hospitali hiyo kwa kuwapokea huku akieleza ushirikiano walionao na NSSF.
Dkt. Msafiri Marijani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar baada ya kupokea Msaada huo wa Vifaa Tiba ameishukuru NSSF kwa msaada huo na kueleza uhitaji walionao katika hispitali hiyo.
Violet Segeja ni Mwenyekiti wa Wanawake wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF katika tukio hilo ametoa wito kwa Jamii hasa wanawake walio katika Vikundi kujiandikisha katika sekta isiyo rasmi katika Mifuko kwa ajili ya manufaa yao ya Baadaye.
Kwa upande wake Mkuu wa Mfuko wa uchangiaji Hiyari – ZSSF Rajabu Haji Machano pamoja na kutoa shukrani kwa mashirikiano na NSSF ametoa wito kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa Hiari.
Hospitali ya Rufaa Mnazi mmoja Zanzibar ni hospitali inayotegemewa na idadi kubwa ya Wananchi hivyo kutolewa kwa msaada huo kutoka NSSF itakuwa ni sehemu ya kuisaidia Jamii kubwa kupata huduma bora zaidi.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *