MCHENGERWA: HAKUNA MSANII MKUBWA KULIKO NCHI

MCHENGERWA: HAKUNA MSANII MKUBWA KULIKO NCHI

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amewataka viongozi wa BASATA na COSOTA kuhakikisha wasanii wote wanasajiliwa hususani wale wakubwa ambao mpaka sasa hawajasajiliwa kwani hakuna msanii mkubwa kuliko Nchi. “Nitoe maelekezo kwa COSOTA na BASATA hatutegemei kusikia wasanii wamesajiliwa wachache, sitegemei kusikia msanii mkubwa hajasajiliwa, tutaanza kuhoji uwezo wa tuliowapa dhamana. “Jukumu letu

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amewataka viongozi wa BASATA na COSOTA kuhakikisha wasanii wote wanasajiliwa hususani wale wakubwa ambao mpaka sasa hawajasajiliwa kwani hakuna msanii mkubwa kuliko Nchi.

“Nitoe maelekezo kwa COSOTA na BASATA hatutegemei kusikia wasanii wamesajiliwa wachache, sitegemei kusikia msanii mkubwa hajasajiliwa, tutaanza kuhoji uwezo wa tuliowapa dhamana.

“Jukumu letu sisi serikali ni kuwaunganisha wasanii wote, hakuna msanii mkubwa kuliko nchi, situliopewa mamlaka twende tuwanyenyekee, wanatoa mchango kwa nchi inanufaika na kupitia kodi.

“Tusijifungie maofisini, twende tukawatafute, kwenye nafasi tuweke watu wenye fani ya sanaa, wasanii wakongwe wapo wanaijua sanaa, tuwateue kwenye nafasi mbalimbali hasa za BASATA ili wakasimamie biashara zao, wakasimamie kutafuta wateja, kuangalia walanguzi na haki zao za msingi.

“Mnaponiletea mapendekezo kwenye mabodi, nileteeni majina ya wasanii, kwa mfano Kenya wanaosimamia ni wasanii wenyewe akina Juakali, na sisi tufanye hivyo ili wakalinde haki zao wenyewe ili kuiendeleza tasnia, hawatakubali sanaa ianguke kwani watakuwa wameanguka wao,” amesema Mchengerwa.



========

UCHAMBUZI

Kauli hiyo ya Waziri inakuja ikiwa ni siku chache tangu Diamond Platnumz na wasani wake wote wa lebo ya WCB kutojisajili katika Tuzo zinazosimamiwa na BASATA, pia ni aliziponda tuzo hizo kwa kusema ‘Kama mirabaha hamtupi mtatupa hizo tuzo’.

Mbali na hapo ni siku chache zimepita tangu Diamond alipozungumza kwa nia ya kukosea kuwa kila anaposafiri nje ya nchi hawezi kuruhusiwa hadi alipe Sh 50,000, ambapo alidai kuwa hajui kama hiyo ni kwa wasanii wote au ni yeye pekee ndiye anayefanyiwa hivyo.

Kwa mwenendo huo ni wazi upepo siyo mzuri baina ya taasisi hizo za Serikali na msanii huyo au lebo yake anayoiongoza.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »