RAIS DK.MWINYI AMEZUNGUMZA WAZIRI MKUU MSTAAFU WA UENGEREZA TONY BLAIR.

RAIS DK.MWINYI AMEZUNGUMZA WAZIRI MKUU MSTAAFU WA UENGEREZA TONY BLAIR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amempongeza Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Tony Balir kwa kutekekeleza kwa vitendo ahadi zake za kuendelea kuiunga mkono Zanzibar hasa katika mipango na mikakati ya upangaji wa vipaumbele kwa watendaji wa Serikali. Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo wakati alipofanya mazungumzo na Waziri

May be an image of 2 people, grandfather clock and indoor
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Tony Blair Ikulu Zanzibar ambaye yupo Zanzibar kwa ziara maalum.
May be an image of 5 people and people standing
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Tony Blair Ikulu Zanzibar ambaye yupo Zanzibar kwa ziara maalum.
May be an image of 2 people, people standing and suit
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakifurahi kwa pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Tony Blair Ikulu Zanzibar ambaye yupo Zanzibar kwa ziara maalum.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amempongeza Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Tony Balir kwa kutekekeleza kwa vitendo ahadi zake za kuendelea kuiunga mkono Zanzibar hasa katika mipango na mikakati ya upangaji wa vipaumbele kwa watendaji wa Serikali.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo wakati alipofanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Tony Blair Ikulu Zanzibar ambaye yupo Zanzibar kwa ziara maalum.

Katika maelezo yake Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Waziri Mkuu Mstaafu Tony Blair kupitia taasisi yake ya (Tony Blair Institute for Global Change), imeweza kuunga mkono jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kutoa mafunzo kwa watendaji wakuu juu ya upangaji wa vipaumbele hatua ambayo ina umuhumu mkubwa katika mipango ya Serikali.

Alisema kuwa mafunzo hayo ambayo Taasisi hiyo iliyatoa kwa watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yana mchango mkubwa katika mipango ya Serikali na utekelezaji wake.

Aidha, Rais Dk, Mwinyi alimuhakikishia kiongozi huyo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuthamini michango ya taasisi ya (Tony Blair Institute for Global Change), kwani imeonesha nia na dhamira kubwa ya kuiunga mkono Zanzibar ili mipango yake ya maendeleo iweze kufanikiwa ipasavyo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »