Makamu wa Rais Dkt. Mpango ameshiriki ufunguzi wa Jukwaa la 8 la Wakuu wa Nchi na Serikali Duniani.

Makamu wa Rais Dkt. Mpango ameshiriki ufunguzi wa Jukwaa la 8 la Wakuu wa Nchi na Serikali Duniani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 29 Machi 2022 ameshiriki ufunguzi wa Jukwaa la 8 la Wakuu wa Nchi na Serikali Duniani linalofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu. Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika jukwaa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 29 Machi 2022 ameshiriki ufunguzi wa Jukwaa la 8 la Wakuu wa Nchi na Serikali Duniani linalofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika jukwaa hilo ambapoPamoja na mambo mengine lina lengo la kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kubadilishana mbinu za kuimarisha utendaji wa serikali.

Katika Ufunguzi wa Jukwaa hilo viongozi wakuu wa serikali, mashirika ya kimataifa pamoja na sekta binafsi kutoka nchi mbalimbali wamekutana na kujadili namna bora ya kuongeza ufanisi katika utoaji huduma za serikali kwa wananchi na kutatua changamoto mbalimbali kupitia utafiti kwa kuzingatia mabadiliko yanayoendelea duniani.

Hapo kesho tarehe 30 Machi 2022 Makamu wa Rais Dkt. Mpango anatarajiwa kuzungumza katika jukwaa hilo akichangia mada ya “kwanini Afrika imekua ni muhimu sana kwa wakati huu katika uchumi wa dunia”

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »