RAIS MWINYI AMEFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA INDIA NCHINI TANZANI

RAIS MWINYI AMEFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA INDIA NCHINI TANZANI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amezipongeza juhudi zinazochukuliwa na Ubalozi wa India nchini Tanzania kwa kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miradi mikubwa ya maji safi na salama. Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo katika mazungumzo kati yake na Balozi wa India

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amezipongeza juhudi zinazochukuliwa na Ubalozi wa India nchini Tanzania kwa kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miradi mikubwa ya maji safi na salama.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo katika mazungumzo kati yake na Balozi wa India katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Binaya Srikanta Pradhan, mazungumzo yaliofanyika Ikulu Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Mwinyi alisema kwamba katika kipindi kifupi tokea balozi huyo kuanza kazi zake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameweza kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi mbali mbali inayotekelezwa Zanzibar kupitia nchi hiyo hatua ambayo inafaa kupongezwa.

Hivyo, Rais Dk. Mwinyi alieleza haja ya kuendelea kufuatilia kwa karibu miradi hiyo ili iweze kutekelezwa kwa wakati uliopangwa ikiwemo miradi mikubwa ya maji safi na salama ambayo ujenzi wake unaendelea.

Akieleza kuhusu uendelezaji wa miradi mikubwa wa maji, Rais Dk. Mwinyi alipongeza hatua zilizofikiwa katika uendelezaji wa miradi hiyo na kueleza matumaini yake ya kukamilika kwa wakati miradi hiyo ambayo inatekelezwa kwa mashirikiano ya pamoja kati ya Benki ya Exim ya India kwa njia ya mkopo wa masharti nafuu kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa upande wa utekelezaji wa rasilimali watu, Rais Dk. Mwinyi aliupongeza mpango wa Serikali ya India wa kutoa nafasi za masomo kwa Tanzania ikiwemo Zanzibar ambapo nafasi hizo za masomo zitadhaminiwa na Serikali ya India.

Aidha, aliipongeza Serikali ya India kwa nia yake ya kuanzisha chuo cha amali kisiwani Pemba na kusema kwamba hatua hiyo itakuwa ni mchango mkubwa hasa kwa vijana walioshindwa kuendelea na elimu ya juu hapa Zanzibar.

Vile vile, alieleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kutoa ushirikiano wake katika azma iliyowekwa na Serikali ya India ya kuanzisha taasisi ya teknolojia ya habari hapa nchini kwani kuwepo kwa taasisi hiyo kutasaidia kuimarisha teknolojia ya habari na mawasiliano nchini.

Mapema, Balozi wa India katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Binaya Srikanta Pradhan, alimueleza Rais Dk. Mwinyi hatua za makusudi zilizochukuliwa na Ubalozi wa nchi hiyo tokea alipokuja Ikulu Zanzibar kujitambulisha mnamo Septemba 16 mwaka jana.

Balozi Pradhan alimueleza Rais Dk. Mwinyi kwamba Ubalozi wa India unathamini uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati yake na Zanzibar hivyo, utahakikisha unaisimamia vyema miradi yote inayotekelezwa na nchi hiyo.

Katika maelezo yake Balozi Pradhan alieleza matarajio yake makubwa na kumuhakikishia Rais Dk. Mwinyi kwamba miradi mikubwa wa maji safi na salama ambayo ujenzi wake unaendelea hivi sasa itakamilika kwa wakati uliopangwa.

Aidha, alitumia fursa hiyo kueleza azma ya Serikali ya India ya kuanzisha kwa chuo cha amali kisiwani Pemba hatua ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kutoa mafunzo ya amali kwa vijana.

Alieleza azma ya Serikali ya India ya kuimarisha uhushaino na ushirikiano wa kibiashara kati yake na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  huku akieleza ujio mkubwa wa wafanyabiashara kutoka nchini humo mwezi Novemba mwaka huu kwa lengo la kuja kuangalia fursa zilizopo Tanzania. Sambamba  na hayo, alisifu mashirikiano mazuri yaliopo kati ya India na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo Zanzibar na kueleza azma ya nchi hiyo ya kujenga kiwanda cha kutengenezea chanjo za maradhi kadhaa hapa nchini.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »