MAONESHO YA MIAKA 58 YA MUUNGANO YAFUNGULIWA

MAONESHO YA MIAKA 58 YA MUUNGANO YAFUNGULIWA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameshiriki katika ufunguzi wa Maonesho ya Miaka 58 ya Muungano uliofanyika katika viwanja vya Maisara Jijini Zanzibar. Akitoa Salamu zake katika Hafla hiyo Mhe. Hemed ameeleza kuwa uwepo wa Muungano huo tayari watanzania wanafahamu dhana ya Muungano na kuendelea kuuzungumza vizuri hasa kwa maslahi

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameshiriki katika ufunguzi wa Maonesho ya Miaka 58 ya Muungano uliofanyika katika viwanja vya Maisara Jijini Zanzibar.

Akitoa Salamu zake katika Hafla hiyo Mhe. Hemed ameeleza kuwa uwepo wa Muungano huo tayari watanzania wanafahamu dhana ya Muungano na kuendelea kuuzungumza vizuri hasa kwa maslahi makubwa yanayopatikana katika pande zote mbili za Muungano.

Aidha Mhe. Hemed ameeleza kuwa Taasisi mbali mbali za Muungano zimekuwa karibu na wananchi ili kuhakikisha wanaelewa zaidi faida zilizomo katika Muungano huo.

Mhe. Hemed amewahakikishia kuwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais itaendelea kusimamia uwepo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa maslahi ya watanzania.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »