RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MWINGINE

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MWINGINE

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa naibu makatibu wakuu wa wizara mbili na kuhamisha wengine watatu. Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Mei 11, 2022 na Mkurugenzi Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Zuhura Yunus imesema kuwa Rais Samia amemteua Dk Charles Msonde kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -Tamisemi (Elimu).

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa naibu makatibu wakuu wa wizara mbili na kuhamisha wengine watatu.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Mei 11, 2022 na Mkurugenzi Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Zuhura Yunus imesema kuwa Rais Samia amemteua Dk Charles Msonde kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -Tamisemi (Elimu).

Dk Msonde amechukua nafasi ya Gerald Mweli ambaye amehamishiwa Wizara ya Kilimo.

Kabla ya uteuzi huu Dk Msonde alikuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta).

Dk Msonde ambaye ameiongoza Necta kwa miaka nane aliteuliwa kushika wadhifa huo Agosti 2014.

Dk Msonde aliteuliwa kushika wadhifa huo kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Profesa Joyce Ndalichako aliyetangaza kuchukua likizo bila malipo kwa ajili ya kujiendeleza kielimu, ambaye kwa sasa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu

Pia, Mkuu huyo wa nchi amemteua Dk Maduhu Kazi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 Dk Kazi amechukua nafasi ya Ramadhani Kailima aliyehamishiwa Tamisemi. Kabla ya uteuzi huu Dk Kazi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC).

Rais Samia pia amefanya uhamisho ambapo Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhan Kailima amehamishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Tamisemi kuchukua nafasi ya Dk Switbert Zakaria Mkama ambaye amehamishiwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano).

Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Gerald Mweli amehamishwa na kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo.

Mwingine aliyehamishwa ni Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Switbert Zakaria Mkama ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais kuchukua nafasi ya Edward Gerald Nyamanga ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi na uhamisho huu umeanza Mei 09, 2002.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »