HALIMA MDEE, WENZAKE WAFUKUZWA RASMI CHADEMA

Baraza Kuu la CHADEMA usiku wa leo kuamkia Alhamisi (Mei 12, 2022) limezitupilia mbali Rufaa za Halima Mdee na wenzake 18 za kupinga kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya chama. Kabla ya kufikia maamuzi hayo Mwenyekiti wa Chadema taifa aliwapa nafasi ya maridhiano na kuwataka waombe radhi mbele ya baraza kuu ili waweze kusamehewa na

Baraza Kuu la CHADEMA usiku wa leo kuamkia Alhamisi (Mei 12, 2022) limezitupilia mbali Rufaa za Halima Mdee na wenzake 18 za kupinga kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya chama.

Kabla ya kufikia maamuzi hayo Mwenyekiti wa Chadema taifa aliwapa nafasi ya maridhiano na kuwataka waombe radhi mbele ya baraza kuu ili waweze kusamehewa na wabakie kuwa wanachama. Lakini kwa kauli moja wote walikataa nafasi hiyo na kusema HAWAPO TAYARI KUOMBA RADHI badala yake wanataka maamuzi yafanyike kwa kura.

Kufuatia maombi yao ya kutaka maaamuzi yafanyike kwa kura, wajumbe wakapewa nafasi ya kupiga kura ambapo wajumbe 413 wametaka akina Halima WAFURUSHWE, wajumbe 4 wametaka WASAMEHEWE, na wajumbe 6 HAWAFUNGAMANI NA UPANDE WOWOTE.

Matokeo ni kama ifuatavyo;
*Kanda ya Victoria Wajumbe 44*-Wanaokubalia wavuliwe uwanachama 42-Wasiokubali 1-Wasiofungamana na Upande  wowote 1_*Jumla kura 44*_
*Kanda ya Nyasa Wajumbe 57*-Wanaokubali wavuliwe uanachama 57-Wasiokubalina 0-Wasifungamana na Upande wowote 0_*Jumla ya Kura 57*_
*Kanda ya Unguja Wajumbe 22*-Wanaokubali wavuliwe uanachama 19-Wasiokubali 1-Wasifungamana na Upande wowote 1_*Jumla ya Kura 22*_


*Kanda ya Pemba 15*-Wanaokubali wavuliwe uanachama 12-Wasiokubali 1-Wasifungamana na Upande wowote 2_*Jumla ya Kura 15*_


*Kanda ya Kusini 32*-Wanaokubali wavuliwe uanachama 32-Wasiokubali 0-Wasifungamana na Upande wowote 0_*Jumla ya Kura 32*_


*Kanda ya Pwani 47*-Wanaokubali wavuliwe uanachama 45-Wasiokubali 0-Wasifungamana na Upande wowote 2_*Jumla ya Kura 47*_


*Kanda ya Kati 44*-Wanaokubali wavuliwe uanachama 44-Wasiokubali 0-Wasifungamana na Upande wowote 0_*Jumla ya Kura 44*_

*Kanda ya Serengeti Wajumbe 41*-Wanaokubali wavuliwe uanachama 41-Wasiokubalina 0-Wasifungamana na Upande wowote 0_*Jumla ya Kura 41*_


*Kanda ya Magharib Wajumbe 37*-Wanaokubali wavuliwe uanachama 37Wasiokubali 0Wasifungamana na Upande wowote 0_*Jumla ya Kura 37*_


*Kanda ya Kaskazini Wajumbe 61*-Wanaokubali wavuliwe uanachama 61-Wasiokubali 0-Wasifungamana na Upande wowote 0*Jumla ya kura 61*


*Kamati Kuu*Wanaokubali wavuliwe uanachama 23Wasiokubali 0Wasiofungamana 0*Jumla ya kura 23*

*Wanaounga mkono wafukuzwe uanachama kura 413*
*Wasiounga mkono kufukuzwa kura 5*
*Wasiofungamana na upande wowote kura 5*

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »