COASTAL UNION YAIFUATA YANGA FAINALI

COASTAL UNION YAIFUATA YANGA FAINALI

Ni rasmi klabu ya Yanga itacheza fainali ya kombe la Shirikisho la Azam hapo Julai 2. Hii ni baada ya Coastal Union FC kutoka Tanga kutinga fainali baada ya kuifunga kwenye mikwaju ya penalti Azam FC 6-5. Mchezo huo umepigwa leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ambapo ambapo timu hizo mpaka dakika

Ni rasmi klabu ya Yanga itacheza fainali ya kombe la Shirikisho la Azam hapo Julai 2.

Hii ni baada ya Coastal Union FC kutoka Tanga kutinga fainali baada ya kuifunga kwenye mikwaju ya penalti Azam FC 6-5.

Mchezo huo umepigwa leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ambapo ambapo timu hizo mpaka dakika 120 zikikuwa hazijafungana na kwenda katika matuta.

Dakika 45 kipindi cha kwanza zilianza kwa kasi huku kila timu ikilishambulia lango la mwenzake lakini papara za washambuliaji wa timu zote zikafanya zikamilike bila kufungana.

Katika vipindi vyote kila timu ilikosa magoli.

Hata katika 30 za nyongeza ilikuwa ngumu ambapo pia zilishindwa kufungana huku Coastal Union FC wakiibuka wababe katika mikwaju ya penati kwa kupata 6-5.

Waliopata penalti kwa Azam FC ni Rodgers Kola, Bruce Kangwa, Never Tigere, Agrey Morris na Idriss Mbombo huku Lusajo Mwaikenda na Charles Zulu wakikosa.

Kwa upande wa Coastal waliopata penati ni Muhsin Makame, Amani Kyata, Pascal Kitenge, William Kising, Moubarack Hamza na Abdul Sopu huku Miraji Hassan akikosa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »