UMEME CHANZO CHA KUUNGUA SOKO LA VETERINARY.

UMEME CHANZO CHA KUUNGUA SOKO LA VETERINARY.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema chanzo Cha Moto uliopelekea kuteketea kwa Soko la Veterinary lililopo TAZARA Wilaya ya Temeke ilitokana na Hitilafu ya umeme. RC Makalla amesema hayo alipotembelea Soko Hilo kujionea uharibifu wa Mali zilizoteketea moto ambapo amesema taarifa za awali zinaonyesha Moto huo umeathiri takribani vibanda 453.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema chanzo Cha Moto uliopelekea kuteketea kwa Soko la Veterinary lililopo TAZARA Wilaya ya Temeke ilitokana na Hitilafu ya umeme.

RC Makalla amesema hayo alipotembelea Soko Hilo kujionea uharibifu wa Mali zilizoteketea moto ambapo amesema taarifa za awali zinaonyesha Moto huo umeathiri takribani vibanda 453.

Aidha RC Makalla amesema Serikali inafanya taratibu za haraka kuhakikisha kazi ya kurejesha Miundombinu iliyoharibika inafanyika usiku na mchana ili Wafanyabiashara warudi kuendelea na Biashara Kama awali ambapo ameahidi hakuna mfanyabiashara atakaeondolewa.

Hata hivyo RC Makalla ametoa pole kwa Wafanyabiashara walioathiriwa na Moto huo na kuwataka kuwa watulivu wakati Serikali yao inaendelea kutatua changamoto hiyo.

Kutokana na matukio ya Moto kujirudia Mara kwa Mara, RC Makalla ameendelea kutoa wito kwa Viongozi wa masoko kuhakikisha kila soko linakuwa na fundi umeme anaetambuliwa na TANESCO,Halmashauri kuweka Vifaa vya kudhibiti moto kwenye Kila soko, Wafanyabiashara kuacha tabia ya kuhinjika maharage jioni ili asubuhi wakute yameiva huku akisisitiza Masoko kuwa na Ulinzi.

MBUNGE AIBUA HOJA KUHUSU MBEGU ZA KIUME BUNGENI

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »