Waziri wa Nchi uwekezaji Mhe Mudrick amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa ILO Bw. Wellington Chibebe.

Waziri wa Nchi uwekezaji Mhe Mudrick amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa ILO Bw. Wellington Chibebe.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imelishukuru shirika la kazi duniani (I.L.O) kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuzipia na kuandaa sera na sheria za ajira nchini ili kuondoa changamoto zinazoikabili sekta hiyo Shukrani hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi, uchumi na uwekezaji Mhe Mudrick Ramadhan Soraga wakati alipokutana na kufanya mazungumzo

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi, uchumi na uwekezaji Mhe Mudrick Ramadhan Soraga akizungumza na Mkurugenzi wa ILO Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Wellington Chibebe ofisi kwakwe Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharib B Unguja
Mkurugenzi wa ILO Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Wellington Chibebe akizungumza na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi, uchumi na uwekezaji Mhe Mudrick Ramadhan Soraga alipomtembelea ofisi kwakwe Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharib B Unguja
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi, uchumi na uwekezaji Mhe Mudrick Ramadhan Soraga akizungumza na Mkurugenzi wa ILO Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Wellington Chibebe ofisi kwakwe Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharib B Unguja

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imelishukuru shirika la kazi duniani (I.L.O) kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuzipia na kuandaa sera na sheria za ajira nchini ili kuondoa changamoto zinazoikabili sekta hiyo

Shukrani hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi, uchumi na uwekezaji Mhe Mudrick Ramadhan Soraga wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa ILO Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Wellington Chibebe ofisi kwakwe Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharib B Unguja

Amesema nia ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuhakikisha inaweka usawa katika sekta ya ajira kwa kupitia  sheria za ajira na usalama wa kazi ambazo zitakwenda sambamba katika utekelezaji ili kuona changamoto za ajira zinapungua kwa waajiri na waajiriwa katika maeneo ya kazi

“Kwasasa tunazipitia sheria zetu za ajira lakini pia masuala ya usalama kwasababu katika sheria hizi huwezi kutekeleza moja na nyingine ukaiacha ni lazima ziende sambamba na hata vipengele vya sera pia vinapaswa kuwa katika mstari mmoja wakati wa kufanya mabadiliko”

Aidha Waziri Soraga amesema serikali ya awamu ya nane ni serikali sikivu na inapenda kushirikiana na wadau wa sekta mbali mbali hivyo ameliomba shirika hilo kuendelea kuunga mkono juhudi za maendelea zinazofanywa na serikali  katika kuimarisha ustawi wan chi na wananchi kwa ujumla

Kwa upande wake Mkurugenzi wa ILO Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Wellington Chibebe amesema wanafurahia ushirikiano uliopo baina ya shirika hilo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa katika sekta ya ajira kutakana kasi ya utekelezaji wa mipango yake  kutokana na kuwepo kwa viongozi makini wanasimamia taasisi hiyo sambamba na kuomba salamu hizo kufikishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi

Kikao hicho ni kufuatia maandalizi ya ushiriki wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mkutano mkuu wa maswala ya kazi uliondaliwa na Shirika la Kazi Duniani (I.L.O) ulioanza tarehe 27 mei na unaotarajiwa kumalizika tarehe 11 juni mwaka huu katika Jiji la Geneva Nchini Uswisi, Ajenda zaidi ya 100 zitajadiliwa katika mkutano huo ikiwmo masuala ya kuweka viwango vya mafunzo kazi kwa wanagenzi (apprenticeship), kazi za staha, usalama na afya kazini, ambapo Zanzibar ni moja kati ya wanufaika wa mafunzo hayo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »