WAKANDARASI WAZAWA NCHINI WAMPONGEZA RAIS SAMIA

WAKANDARASI WAZAWA NCHINI WAMPONGEZA RAIS SAMIA

Na Barnabas Kisengi, Dodoma Chama vha wakandarasi Tanzania wanatarajia kufanya kongamano la  kumpongeza RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kwa kupokea tunzo ya usimamizi na utekelezaja wa miundombinu bora hapa nchini. Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dodoma Mwenyekiti wa chama cha Wakandarasi nchini  THOBIAS KYANDO amesema watakuwa na kongamano la kujadili mambo mbalimbali

Na Barnabas Kisengi, Dodoma

Chama vha wakandarasi Tanzania wanatarajia kufanya kongamano la  kumpongeza RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kwa kupokea tunzo ya usimamizi na utekelezaja wa miundombinu bora hapa nchini.


Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dodoma Mwenyekiti wa chama cha Wakandarasi nchini  THOBIAS KYANDO amesema watakuwa na kongamano la kujadili mambo mbalimbali ya Wakandarasi hapa nchini kwa kumpongeza Rais Samia kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara hapa nchini.


Adha KYANDO amesema wanaiomba Serikali kuhakikisha inakuwa inawashirikisha wakandarasi wazawa katika miradi mikubwa inayotekelezwa na makampuni kutoka nje kwani itawajegea uwezo mkubwa pindi makampuni hayo yakiondoka.


Kwa upande wake Mkandarasi Mwanamke BI. MAIDA WAZIRI ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na MHE. SAMIA SULUH HASSAN Kwa kuwakikisha inawapa kipaombele wakandarasi wanawake wazawa kupata kazi mbalimbali za miradi hapa nchini hivyo wao kama wanawake watahakikisha hawamuangushi Mheshimiwa Rais katika utekelezaji wa miradi hapa nchini.


Kongamano hilo la kumpongeza Rais Samia litafanyika kesho Juni 04, 2022 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete convention uliopo Jijini Dodoma ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Ujenzi Prof Makame Mbarawa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »