RAIS SAMIA APIGA SIMU, AONGEA NA WAKANDARASI WAZAWA KWENYE KONGAMANO LA KUMPONGEZA

RAIS SAMIA APIGA SIMU, AONGEA NA WAKANDARASI WAZAWA KWENYE KONGAMANO LA KUMPONGEZA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Amewataka Wakandarasi wazawa hapa nchini kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia waledi na uzalendo kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao ili serikali iendelee kuwaamini katika kuwapa miradi malimbali inayoendelea kujengwa.Kauli hiyo ameitoa leo wakati alipowapigia simu na kuwapa maelekezo hayo wakati wa kongamano la wakandarasi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Amewataka Wakandarasi wazawa hapa nchini kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia waledi na uzalendo kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao ili serikali iendelee kuwaamini katika kuwapa miradi malimbali inayoendelea kujengwa.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati alipowapigia simu na kuwapa maelekezo hayo wakati wa kongamano la wakandarasi wakimpongeza Rais Samia Kwa kutunukiwa tuzolewa ya usimamizi bora wa miradi ya miundombinu.


Akizungumza na Wakandarasi hao Naibu Waziri wa Ujenzi Godfrey Kasekenya amesema wakandarasi wanapaswa kuzingatia maelekezo waliyopewa na Rais ili Serikali iendelee kuwaamini na kuwapa kazi kila wakati.


Kwa upande wake Meneja wa Tarura Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Geoffrey Nkinga aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Tarura amesema Serikali kwa sasa inamiradi mingi ya barabara za mjini na vijinini hivyo wakandarasi wanatakiwa kufanya kazi kwa kuhakikisha wanatanguliza uzalendo na kufanya kazi bora na kwa wakati ili serikali ihakikishe inakuwa na imani na Wakandarasi wazawa.


Adha Nkinga Amewataka Wakandarasi wazawa kuhakikisha wanakuwa mbele kujitokeza katika zabuni mbalimbali zinazokuwa zinatangazwa na Serikali za miradi mbalimbali ya ujenzi hapa nchini.


Mwenyekiti wa Wakandarasi hapa nchini Eng Thobias Kyando ameishukuru Serikali kwa kuwa imekuwa inawapa ushirikiano mkubwa Wakandarasi wazawa ambopo hadi sasa sekta ya Wakandarasi inazidi kukuwa kutoka Wakandarasi 830 na wanategemea ifikapo mwisho wa mwaka huu kuwa na zaidi ya Wakandarasi wazawa 1500.


Kongamano la Wakandarasi hao la kumpongeza Rais Samia limefanyika Jijini dodoma na kuhudhuriwa na viongi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »