WAZIRI DKT. GWAJIMA AANZIA MTAANI KWAKE VITA DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA NA WATOTO

WAZIRI DKT. GWAJIMA AANZIA MTAANI KWAKE VITA DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA NA WATOTO

Na Mwandishi Wetu- Dodoma. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalum, Dkt Dorothy Gwajima, ameripoti kwa viongozi wa mtaa wake anaoishi wa Ilazo Mbuyuni kwa lengo la kukutana na kujadiliana na viongozi hao wa Mtaa wa Ilazo Mbuyuni, Kata ya Ipagala jijini Dodoma ili kuweka mbinu za kukabilina na ukatili wa kijinsia

Na Mwandishi Wetu- Dodoma.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalum, Dkt Dorothy Gwajima, ameripoti kwa viongozi wa mtaa wake anaoishi wa Ilazo Mbuyuni kwa lengo la kukutana na kujadiliana na viongozi hao wa Mtaa wa Ilazo Mbuyuni, Kata ya Ipagala jijini Dodoma ili kuweka mbinu za kukabilina na ukatili wa kijinsia kwenye jamii ikiwemo ukatili kwa watoto. 

Akizungumza na Uongozi wa Kata hiyo Juni 23, 2022, Dkt. Gwajima amesema mbinu za kutokomeza Ukatili lazima zitokane na Wanajamii wenyewe kwa sababu wanaofanya ukatili wanatoka miongoni mwao.  “Sisi Wanajamii ya Ipagala lazima tuungane na jamii ya watanzania wote kuitikia wito wa Serikali katika kupambana na ukatili na ikiwezekana tuwe wa kupigiwa mfano na jamii zingine” amesema Dkt. Gwajima. 

Kuhusiana na takwimu za ukatili, Waziri Dkt Gwajima alisema, matukio yaliyoripotiwa kwa mwaka 2021 yalikuwa zaidi ya 11000 kwa watoto, huku matukio ya ubakaji yakiwa zaidi ya 5000. 

Kufuatia mchango alioutaka wa Mhe. Waziri Gwajima juu ya Mbinu gani zitumike kukabiliana na ukatili kama mchango wao, Diwani wa Kata ya Ipagala, Gombo Kamuli, alimuomba Mhe. Waziri awapatie muda wakae kama Kamati ya Ushauri ya Kata kisha watatoka na mapendekezo ya mbinu za kutumia kukabiliana na Ukatili kulingana na aina ya ukatili.  “Mhe Waziri sisi tunaahidi tutakaa kwa pamoja kama viongozi wa Kata tufanye tathmini ya ukubwa tatizo kwenye kata yetu kisha tutoke na maazimio ambayo tutayafikisha kwako ili kupata ushirikiano zaidi” Alisema Mhe. Gombo.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilazo Mbuyuni Lucas Mwasongwe, alimpongeza Waziri kwa kushuka na kujadili suala hilo katika ngazi ya chini na kuwaomba viongozi kuiga mfano huo.

Mwenyekiti huyo wa Mtaa aliiasa jamii kuwa karibu na Watoto wao na kuchunguza mienendo yao hususani walio kwenye Shule za Bweni. “Mtoto akitoka Shule kaa naye, mdadisi mfanye kuwa Rafiki, Kataeni Vitendo vya Ukatili vimekithiri kama alivyosema Mhe. Waziri” alisema Mwasongwe.

 Waziri Dkt. Gwajima, amekuwa akifanya ziara kwenye maeneo mbali mbali nchini akiwa na lengo lakuhakikisha zinapatikana mbinu mbadala kukabiliana na changamoto ya ukatili nchini na safari hii ikiwa ni kwenye mtaa anaoishi yeye mwenyewe wa Ilazo Mbuyuni.  

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »