GEITA GOLD YAFUNGIWA NA FIFA/ TFF WATOA NENO

GEITA GOLD YAFUNGIWA NA FIFA/ TFF WATOA NENO

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeifungia klabu ya Ligi Kuu ya NBC ya Geita Gold kusajili wachezaji hadi itakapomlipa aliyekuwa Kocha wake Ettiene Ndayiragije. Kocha huyo raia wa Burundi alifungua madai dhidi ya Geita Gold FC akidai fidia ya kuvunjiwa mkataba pamoja na malipo mengine wakati akiifundisha timu hiyo ya mkoani Geita.

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeifungia klabu ya Ligi Kuu ya NBC ya Geita Gold kusajili wachezaji hadi itakapomlipa aliyekuwa Kocha wake Ettiene Ndayiragije.

Kocha huyo raia wa Burundi alifungua madai dhidi ya Geita Gold FC akidai fidia ya kuvunjiwa mkataba pamoja na malipo mengine wakati akiifundisha timu hiyo ya mkoani Geita.

Kwa mujibu wa taratibu za FIFA, iwapo Geita Gold FC itakuwa haijamlipa Kocha huyo, suala hilo litawasilishwa katika Kamati ya Nidhamu ya FIFA kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linazikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zinaingia na wachezaji pamoja na makocha, kwani hiyo ni moja ya vigezo vya kupata Leseni ikiwa ni utekelezaji wa Kanuni ya Leseni za Klabu (Club Licensing Regulations).

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »