MAFUNZO YA SENSA YAMEANZA RASMI LEO

MAFUNZO YA SENSA YAMEANZA RASMI LEO

Na Barnabas Kisengi Dodoma Mafunzo ya SENSA katika ngazi ya Mikoa yanayowashirikisha wataalamu kutoka Tamisemi pamoja na waratibu wa SENSA wa Wilaya, Maafisa Elimu Mikoa na wilaya, wataalamu wa Tehama wa Wilaya, Maafisa mipango wilaya,Maafisa Maendeleo Jamii wilaya, Waratibu Elimu kata pamoja na wawakilishi kutoka vyama vya watu wenyeulemavu yameanza kufanyika leo hapa nchini ambayo

Na Barnabas Kisengi Dodoma


Mafunzo ya SENSA katika ngazi ya Mikoa yanayowashirikisha wataalamu kutoka Tamisemi pamoja na waratibu wa SENSA wa Wilaya, Maafisa Elimu Mikoa na wilaya, wataalamu wa Tehama wa Wilaya, Maafisa mipango wilaya,Maafisa Maendeleo Jamii wilaya, Waratibu Elimu kata pamoja na wawakilishi kutoka vyama vya watu wenyeulemavu yameanza kufanyika leo hapa nchini ambayo yataifanya kwa siku 21 katika mikoa yote hapa nchini.


Kauli hiyo imetolewa leo Julai 06 2022  na MTWAKAIMU MKUU WA SERIKALI Dkt ALBINA CHUWA wakati Akizungumza na waandishi wa habari Ofisin kwakwe jijini dodoma.


Dkt. CHUWA amesema kuwa mafunzo hayo yameanza leo baada ya kumalizika mafunzo kwa ngazi ya Taifa yaliyofanya kwa siku 21 ambayo yalianza Juni 10 hadi Juni 30 mwaka huu ambapo leo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo na uelewa wa pamoja washiriki wote kuhusu nyenzo zote za SENSA ya watu na makazi, SENSA ya Majengo na SENSA ya Anwani za Makazi.


Mtwakwimu Mkuu amesema baada ya mafunzo hayo ngazi ya Mikoa washiriki watakao faulu watakuwa na wajibu wa kwenda kufundisha wasimamizi na makarani wa SENSA wapatao ngazi ya wilaya, Tarafa na shehia kwa muda wa siku 21 kuanzia Julai 29  hadi Agust 18 mwaka huu kabla ya kufikia usiku wa SENSA agost 23. 


Dkt.CHUWA amesema kuanzia Julai 6 hadi 26 kamati za SENSA Katika ngazi ya wilaya, kata, Mitaa, Vijiji na shehia watakuwa na jukumu kubwa la kukamilisha mchakato wa ajira za makarani na wasimamizi wote Nchi nzima na kuhakikisha kuwa makarani wote wapatao 205,000. Wanatoka katika maeneo wanayoishi.


Aidha Mtwakwimu Mkuu wa Serikali Dkt CHUWA amesrma maandalizi ya SENSA ya Mwaka huu hadi sasa wamefikia asilimia 87 na akaelezea SENSA zilizopita kuwa SENSA ya kwanza hapa nchini ilianza mwaka 1967 ambapo kulikuwa na watanzania zaidi ya milioni 12, SENSA ya pili ilifanyika mwaka 1978 ambapo watanzania walikuwa zaidi ya milioni 17, SENSA ya tatu ilifanyika Mwaka 1988 ambapo watanzania zaidi ya milioni 23, na SENSA ya nne ilifanyika Mwaka 2012 ilikuwa na zaidi watanzania milioni 44 na sasa Agost 23  mwaka huu Tanzania inafanyika SENSA ya Tano.


Dkt. CHUWA Amewataka wanahabari kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanaelimisha Jamii juu yaeumuhimu wa kuhesabiwa huku akiwatoa hofu watanzania kujitokeza kuhesabiwa ifikapo Agost 23 mwaka huu na Amesisitiza kutakuwa naeusiri mkubwa kwa karani wa SENSA na mkuu wa kaya pindi zoezi hilo la SENSA litakapo fanyika huku akiwasisitiza wahusika wote kuhakisha wanafuata maelekezo waliyopewa kwenye mafunzo waliyopewa.
“Niwatoe hofu watanzania juu ya usiri wa zoezi la SENSA makarani wetu wamepatiwa mafunzo ya kutosha pia watakuwa wamekula kiapo cha mahakama hivyo hali ya usiri mkubwa itakuwepo na karani yoyote atakaye kwenda kinyume na miongozo aliyopewa sheria zetu ziko wazi tu kwa kutumikia kifungo cha zaidi ya miaka miwili jela ila nawakilisha watanzania kuwa zoezi letu la SENSA litakwenda vizuri’ Alisisitiza Dkt.CHUWA


Kauli mbiu mwaka huu ni ” SENSA KWA WOTE JIANDAE KUHESABIWA”

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »