WATUMISHI WAWILI KITENGO ARDHI JIJINI DODOMA WAFUKUZWA KAZI

WATUMISHI WAWILI KITENGO ARDHI JIJINI DODOMA WAFUKUZWA KAZI

Na Barnabas Kisengi-Dodoma Watumishi wawili wa kitengo cha ardhi katika Jiji la Dodoma wamefukuzwa kazi na wengine watano wamesimamishwa kwa kusababisha migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano, Julai 07 2022 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa jiji Joseph Mafuru katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha Mkoa kilipokutana na watumishi wapya

Na Barnabas Kisengi-Dodoma


Watumishi wawili wa kitengo cha ardhi katika Jiji la Dodoma wamefukuzwa kazi na wengine watano wamesimamishwa kwa kusababisha migogoro ya ardhi.

Joseph Mafuru
Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma


Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano, Julai 07 2022 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa jiji Joseph Mafuru katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha Mkoa kilipokutana na watumishi wapya wa idara ya ardhi.

Mhe. Anthony Mtaka
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao hicho kilichokuwa kikijadili mikakati ya kumaliza migogoro ambayo imetajwa kukita mizizi na kulifanya jiji hilo liongoze kwa migogoro.
Katika kikao hicho, Mafuru amesema sababu iliyowaingiza matatizoni watumishi hao ni uuzaji na viwanja na kubadili matumizi ya maeneo kwa lengo la kujipatia kipato.
“Mfano mzuri ni eneo lile la Mwanga Bar, tangu 1978 ni eneo wazi lakini mtu ghafla kaibuka na kubadili matumizi yake eti akapima viwanja na watu wakaanza kujenga, hilo ni tatizo,” amesema Mafuru.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amesema hatawavumilia watumishi wanaosababisha migogoro ya mara kwa mara kwakuwa wanawafanya watumishi wengine washindwe kuwahudumia wananchi na kutumia muda mwingi zaidi kutatua au kuendesha mazungumzo ya migogoro.


Mtaka amewataka watumishi waliohamia katika jiji hilo kuwa makini na waache tamaa ya utajiri wa haraka kwa kuwa wanawataza kwa jicho pana.
Katika mkutano huo, Mtaka amemsifu  Kamishna wa Ardhi kwa kuigawa Dodoma katika kanda ambapo itakuwa  rahisi kupunguza migogoro ya wananchi ambayo mingi imesababishwa na maamuzi ya baadhi ya watendaji Serikali.


Kuhusu utoaji wa viwanja kwa zaidi ya mtu amesema kuna shida kubwa na wengi wanalalamika jambo hilo akiwataja wakuu wa mikoa ya Songwe na Mbeya kwamba wamelizwa viwanja vyao na tayari kuna watu wanajenga.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »