NDEJEMBI: TAKUKURU WATATUPA MAJIBU JUMAMOSI

NDEJEMBI: TAKUKURU WATATUPA MAJIBU JUMAMOSI

Na Barnabas Kisengi-Chamwino NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Deo Ndejembi amewaahidi wananchi wa Kijiji cha Mahama kilichopo Kata ya Chilonwa kuwa watendaji wote watakaothibitika kuhusika na ubadhirifu wa fedha za ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho watachukuliwa hatua kali za kisheria na kinidhamu. Ndejembi ameyasema hayo wakati wa

Na Barnabas Kisengi-Chamwino

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Deo Ndejembi amewaahidi wananchi wa Kijiji cha Mahama kilichopo Kata ya Chilonwa kuwa watendaji wote watakaothibitika kuhusika na ubadhirifu wa fedha za ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho watachukuliwa hatua kali za kisheria na kinidhamu.

This image has an empty alt attribute; its file name is WhatsApp%20Image%202022-07-07%20at%207.42.53%20PM.jpeg



Ndejembi ameyasema hayo wakati wa muendelezo wake wa ziara ya kuzungumza na Wananchi wake ambapo ametembelea Kata za Chilonwa na Membe.

” Nilifanya ziara ya kutembelea ujenzi wa Zahanati ya Mahama na sikuridhishwa na kushindwa kukamilika kwake licha ya Serikali yetu kutupatia Sh Milioni 50 kwa ajili ya kumalizia ujenzi huu, niliagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi na wameniambia kuwa tayari wameshakamilisha uchunguzi wao.

This image has an empty alt attribute; its file name is WhatsApp%20Image%202022-07-07%20at%207.42.54%20PM.jpeg

This image has an empty alt attribute; its file name is WhatsApp%20Image%202022-07-07%20at%207.42.53%20PM%20(1).jpeg



Jumamosi nitafika hapa na Kamanda wa TAKUKURU wa Wilaya na Timu ya wataalamu wa Halmashauri yetu ili atueleze kipi wamekigundua kwenye uchunguzi wao na yeyote ambaye atahusika na kushindwa kukamilika kwa ujenzi huu sheria itafuta mkondo wake.

This image has an empty alt attribute; its file name is WhatsApp%20Image%202022-07-07%20at%207.42.55%20PM%20(1).jpeg


Haiwezekani wenzetu wa Haneti wamalize ujenzi wao kwa kiasi sawa na hiki kilicholetwa hapa Mahama halafu hapa ishindikane, hatuwezi kuruhusu kuona fedha ambazo Rais Samia amezileta kwa ajili ya wananchi zinatumiwa vibaya na kushindwa kufanya kazi iliyokusudiwa, tutachukua hatua,” Amesema Ndejembi.

Ndejembi amesema kukamilika kwa vyumba Saba vya madarasa katika Shule Shikizi ya Mchoya kumempa nguvu ya kuiomba Serikali iweze kuithibitisha Shule hiyo kuwa Shule kamili ili iweze kumaliza changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda katika Shule ya Nzala ambayo iko kitongoji kingine.

” Niliwaahidi wakati naomba kura hapa kwamba Mchoya wanafunzi hawatokaa tena chini kwenye Shule hii Shikizi, leo nina furaha kuona kwamba tumekamilisha ujenzi wa madarasa Saba na sasa ni jukumu langu kuiomba Serikali itupitishie iwe Shule kamili.

Tunamshukuru Rais Samia kwani kupitia yeye tulipata kiasi cha Sh Milioni 80 za fedha za Uviko-19 ambazo zimetusaidia kupata vyumba hivi, Sasa wanafunzi wetu hawatotembea tena umbali mrefu kwenda Nzali,” Amesema Ndejembi.

This image has an empty alt attribute; its file name is WhatsApp%20Image%202022-07-07%20at%207.42.55%20PM.jpeg



Akizungumza na wananchi wa Kata ya Membe Kijiji Cha Mlimwa, Ndejembi amemshukuru Rais Samia kwa kuwezesha kumaliza changamoto ya Maji iliyokuepo kwa muda mrefu sambamba na kufanikisha robo ya vitongoji vya Kata hiyo kufikiwa na umeme.

” Hapa Mlimwa hatukua na Maji lakini sasa Serikali imetupatia mradi wa maji, umeme pia umetufikia kwenye robo ya vitongoji vya Kijiji chetu naamini kwa upendo alionao Mama Samia kwetu vijiji vyote vilivyobaki vitawaka umeme,” Amesema Ndejembi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »