NAIBU KATIBU MKUU MMUYA: WANANCHI WAYAFURAHIA MAISHA MAPYA YA MSOMERA

NAIBU KATIBU MKUU MMUYA: WANANCHI WAYAFURAHIA MAISHA MAPYA YA MSOMERA

Na Mwandishi Wetu-Handeni. Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Kaspar Mmuya akikabidhi hati miliki ya maeneo kwa ajili ya makazi na mashamba kwa wananchi waliowasili katika eneo la Msomera Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga Julai 7, 2022. Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)

Na Mwandishi Wetu-Handeni.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Kaspar Mmuya akikabidhi hati miliki ya maeneo kwa ajili ya makazi na mashamba kwa wananchi waliowasili katika eneo la Msomera Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga Julai 7, 2022.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Kaspar Mmuya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe wakikagua moja ya hati miliki kabla ya zoezi la kugawa kwa wakazi wapya wa eneo la Msomera waliohamia kwa hiari kutoka katika eneo la Hifadhi la Ngorongoro.

NA. MWANDISHI WETU

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Bw. Kaspar Mmuya amewashukuru wananchi waliohamia katika Kijiji cha Msomera awamu ya nne huku wakionesha furaha yao kwa kuanza maisha mapya ya katika kijiji hicho.

Ametoa pongezi hizo Julai 7, 2022 wakati wa zoezi la kuwapokea wananchi walihamia kwa hiari katika kijiji cha Msomera Wilayani Handeni kutoka katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha ikiwa ni kundi la nne toka zoezi hilo kuanza.

Alieleza kuwa katika awamu hiyo wamewasili jumla ya wananchi 188 wakiwa wenye furaha na kupongeza Serikali kwa uratibu mzuri wa zoezi hilo huku wakitarajia kuishi kwa amani na kuendelea na shughuli zao za kila siku.

Aidha Mmuya alitumia fursa hiyo kuwaasa wananchi kutumia maeneo hayo kimkakati kwa kuanza kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo ikiwemo ufugaji wa kisasa utakao chagiza ongezeko la kipato kwa wakazi hao wapya.

“Kipekee namshukuru Rais wetu mpendwa Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha zoezi hili kufanyika kwa weledi mkubwa na hii inaonesha namna Serikali yenu inavyowajali, tunawaahidi tutaendelea kushirikiana na zitumieni fursa zilizopo Msomera,”alisema Mmuya

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe akizungumza wakati wa zoezi hilo alisema Wilaya yake imejipanga kuhakikisha inatoa ushirikiano usiku na mchana huku akiwahakikishia wananchi wote waliohamia katika eneo hilo watapata huduma zote muhimu ambapo amewasihi kubadili mitazamo na kujua kuwa wamekuwa wakazi rasmi wa Msomera.

Pia aliwataka kuhakikisha wanapeleka watoto shule kwa kuzingatia ni jambo muhimu na kuahidi kufanya sense ya kuhakikisha kila mtoto mwenye sifa ya kwenda shule anapelekwa ili kuwa na kizazi chenye elimu na kujikwamua kimaisha.

“Tujenge kizazi chetu hapa msomera chenye elimu, na mimi huu utakuwa ni wimbo wangu, hakikisheni mnapelekea watoto shule na nitafanya sense ya kuhakikisha kila mtoto anapata haki ya elimu,”alisema

Akitoa kauli ya ukiri wa kupokea wananchi na mifugo kwa awamu hiyo ya nne alisema mifugo yote itakayokuwa eneo hilo itunzwe na kuhakiksha inahudumiwa vyema ili ilete manufaa kwao na wakazi wengine wa Handeni hata nje ya hapo.

“Hadi leo ninakiri kumepokea jumla ya kaya 104 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, idadi ya watu 690 ikiwemo watoto 102, ila kwa awamu hii ya nne nimepokea idadi ya watu 188 ambapo148 ni watu wazima na 40 ni watoto ,upande wa mifugo ninakiri kupokea jumla ya mifugo ikiwemo;  ng’ombe 240, mbuzi 348, punda 22, kondoo 274 kwa ujumla ya idadi za mifugo toka awamu ya kwanza tumepokea jumla ya ng’omba 638, kondoo 516 na mbuzi 836 mifugo hii itunzwe na kuhakiksha inahudumiwa kwa usahihi,”alisisitiza Mhe Mchembe.

Naye Aliyekuwa Diwani ya Kakesio kutoka Ngorongoro Mhe. Johannes Tiamasi akitoa neno la shukran aliendelea kupongeza namna zoezi lilovyoearibiwa huku akiwasihi viongozi wenzake waliobaki Ngorongoro kuacha kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu maeneo ya Msomera ikiwemo dhana potofu juu ya zoezi zima la kuhamia katika eneo hilo.

“Msomera ni nzuri sana, ardhi ni nzuri niwatoe hofu waliobaki Ngorongoro kujiandikisha kwa kuzingatia nafasi ya kufanya hivyo bado ipo, hakika hili ni eneo la maziwa na asali hivyo tulikimbilie,”alisisitiza Tiamasi

Naye Mwenyekiti wa Msomera Bw. Martine Oleikayo Paraketi alieleza kwamba wataendelea kutoa ushirikiano kwa uongozi uliopo huku akiwaasa wananchi hao kuiona msomera yeye mazingira rafiki katika kila sekta ikiwemo uwepo wa miundombinu ya maji, mawasiliano, umeme, afya na elimu.

“Msomera kumenoga kwani kuna kila huduma muhimu tunayohitaji hivyo tujisikia vizuri kuwepo hapa na tuendelee kuishi kwa amani na upendo kwa kuzingatia nchi yetu ni kitovu cha amani tuijenge msomera yetu iwe ya mfano kwa wengine,”alisema Oleikayo

Baadhi ya wananchi waliohamia kwa hiari katika eneo la Msomera Wilayani Handeni kutoka katika Hifadhi ya Ngorongoro wakiwasili rasmi katika kijiji hicho Mkoani Tanga Julai 7, 2022.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe akizungumza wakati wa hafla ya kuwapokea kwa hiari katika eneo la Msomera Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga Julai 7, 2022.

Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kakesiyo kutoka Ngorongoro Mhe. Johannes Tiamasi akitoa neno la shukrani mara baada ya mapokezi ya wananchi 188 waliohamia awamu ya nne katika eneo la Msomera Handeni Tanga.

Baadhi ya wananchi waliohamia kwa hiari katika eneo la Msomera Wilayani Handeni Mkoani Tanga wakifuatilia kikao mara baada ya kuwasili rasmi katika eneo hilo.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »