JESHI LA POLISI DODOMA LINAMSHIKILIA KADA WA CHADEMA ‘TWAHA MWAIPAYA’

JESHI LA POLISI DODOMA LINAMSHIKILIA KADA WA CHADEMA ‘TWAHA MWAIPAYA’

Na Barnabas Kisengi-Dodoma Jeshi la polisi mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa watatu, akiwemo mratibu wa uhamasishaji wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA taifa, Twaha Mwaipaya kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kwenye ukurasa wake wa twiter kuhusiana na kupanda kwa bei za umeme. Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoa

Na Barnabas Kisengi-Dodoma


Jeshi la polisi mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa watatu, akiwemo mratibu wa uhamasishaji wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA taifa, Twaha Mwaipaya kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kwenye ukurasa wake wa twiter kuhusiana na kupanda kwa bei za umeme.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma MARTINE OTIENO, amewataja watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa na jeshi hilo kuwa ni FRANK TYPHONE na CHARLES MASANJA mkazi wa Tunduma mkoani Songwe ambao kwa pamoja walikuwa wakijihusisha na matukio ya utapeli wa mitandaoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma MARTINE OTIENO


  OTIENO amesema baadhi ya vitu vilivyokamatwa katika operesheni mbalimbali vikiwemo laptop 7, pikipiki 25, ving’amuzi 3, Milango 22, copper waya na bangi pamoja na mbegu zake. Amewataka watu walioibiwa pikipiki wake na vielelezo kuangalia pikipiki hizo kama ni zao wake wachukuwe.

Kamanda OTIENO amesrma Operesheni dhidi ya vitendo vya uhalifu katika mkoa wa Dodoma iliyofanywa na jeshi la polisi mkoa umefanikiwa kunasa jumla ya watuhumiwa 42, huku kamanda OTIENO akitumia wasaa huo kuwahakikishia usalama wakazi wa mkoa huo katika kusherehekea sikukuu ya Eid El Hajj.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »