NEC YATANGAZA MBUNGE MPYA

NEC YATANGAZA MBUNGE MPYA

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania, imemteua Tamima Haji Abass kuwa Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Julai 9, 2022 na Tume hiyo imesema imemteua mbunge huyo mpya baada ya kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Tanzania ya kuwepo kwa nafasi wazi

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania, imemteua Tamima Haji Abass kuwa Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Julai 9, 2022 na Tume hiyo imesema imemteua mbunge huyo mpya baada ya kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Tanzania ya kuwepo kwa nafasi wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, Irene Ndyamkama.

“Uteuzi huo umefanyika baada ya Tume kupokea barua ya tarehe 12 Mei, 2022 kutoka kwa Spika wa Bunge iliyoandikwa kwa mujibu wa kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 ikitarifu kuhusu uwepo wa nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Irene Alex Ndyamkama” imesema taarifa hiyo ya NEC

“Kwa Kuzingatia matakwa ya ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 ikisomwa pamoja na kifungu cha 86A (6) na (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 imemteua Tamima Haji Abass kuwa Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi” imesema taarifa hiyo.

Irene alifariki dunia Aprili 24, 2022 katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha mkoani Pwani alikokuwa akipatiwa matibabu ambapo aliacha mtoto mchanga.

Hata hivyo baada ya siku saba mbunge huyo kufariki dunia, mtoto mchanga aliyemuacha naye alifariki dunia.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »