MHE. SIMBACHAWENE, BARABARA YA MAKOSE IDODOMA ITAKARABATIWA

MHE. SIMBACHAWENE, BARABARA YA MAKOSE IDODOMA ITAKARABATIWA

Na Barnabas Kisengi-Mpwapwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema serikali kupitia Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa imetenga fedha kiasi cha million 626 kukarabati na kutengeneza katika barabara ya Makose kwenda Idodoma.  “Umbali wa km 25 wa kipande cha barabara utachongwa, km 21 zitawekwa changarawe na km1

Na Barnabas Kisengi-Mpwapwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema serikali kupitia Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa imetenga fedha kiasi cha million 626 kukarabati na kutengeneza katika barabara ya Makose kwenda Idodoma.

 “Umbali wa km 25 wa kipande cha barabara utachongwa, km 21 zitawekwa changarawe na km1 kitawekwa lami ya zege. Tayari bajeti ilishatengwa katika mwaka uliopita wa fedha wa serikali itaweka fedha nyingine kwa mwaka huu wa fedha kwa ajili ya kutengeneza barabara hiyo”

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George simbachwene amesema hayo katika mkutano wa hadhara kata ya Mlalo jimbo la Kibakwe Wilayani ya Mpwapwa.

“Fedha ya Mwaka huu itatumika kuchomoa mawe katika eneo la barabara na itamwaga kifusi na pia kuweka zege  katika maeneo mengine makorofi,amesema “waziri Simbachawene

Aidha Waziri Simbachawene amehimiza wananchi kupitia serikali za vijiji kujenga utaratibu wa kukagua na kurudishia barabara pale inaponesha imebomoka, ni lazima tutunze barabara zetu zote.

Awali Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpwapwa  Mhe. George Fuime na diwani wa kata ya Mpwapwa mjini amesema Halmashauri ina mpango wa kutengeneza sheria ndogo ya kukarabati majengo yote chakavu ya shule za msingi ili kujenga mazingira bora ya kujifunzia kwa wanafunzi Wilayani Mpwapwa.

“Tutatunga sheria ndogo pia ya kuhifadhi vyanzo vya maji ili wananchi wasishughulike na shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka eneo la chanzo cha maj ili uoto uliopo uendelee kubakia kama ulivyo”alisisitiza Fuime.

Pia Mwenyekiti huyo wa Halmashauri ya Wilaya amewataka wananchi wa Jimbo la kibakwe kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika usiku wa SENSA ya watu na Makazi ifikapo Agost 23 mwaka huu ili kila moja ahakikishe amehesabiwa na kuifanya Serikali kuweza kupanga mipango ya Maendeleo vizuri hapa nchini.

Ziara ya Mh waziri Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la kibakwe ni mwendelezo wa kukutana na Wananchi Jimboni kwake kwa kutatua kero mbalimbali na kupanga mipango ya Maendeleo Katika jimbo la kibakwe

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »