WAZIRI SIMBACHAWENE AFANYA ZIARA JIMBONI KWAKE KIBWAKWE

WAZIRI SIMBACHAWENE AFANYA ZIARA JIMBONI KWAKE  KIBWAKWE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi wa kata ya Mangaliza katika mkutano wa hadhara alioufanya katika jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Mpwapwa. Na Mwandishi wetu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameagiza Halmashauri ya wilaya

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi wa kata ya Mangaliza katika mkutano wa hadhara alioufanya katika jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Mpwapwa.

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameagiza Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa kuisajili kwa wakala wa barabara vijijini TARURA barabara ya Kikuyu  Mangaliza kuelekea Kijiji cha Kilambo.

“tujenge misingi imara katika kutekeleza miradi ya maendeleo ili tuimarishe ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, miundo mbinu ya afya na miundo mbinu ya elimu”

Hayo yamesemwa na    Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene alipokuwa anazungumza na wananchi wa kata ya Mang’aliza katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Mpwapwa

Pia Waziri Simbachawene amewasisitiza Wananchi kuhakisha wanajitokeza ifikapo Agost 23 wanajitokeza kwenye zoezi la SENSA kuhesabiwa ili Serikali iweze kupanga mipango ya Maendeleo katika maeneo yao.

Simbachawene ameendelea na ziara yake ya kikazi kwa Wananchi wa Jimbo lake la kibakwe kwa kufanya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo na kufanya mikutano ya hadhara kwa kuzungumza na wananchi wa kata ya Mang’aliza Jimboni kibakwe Wilayani Mpwapwa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »