RAIS DKT. MWINYI KUANZA ZIARA KATIKA MIKOA MITANO ZANZIBAR

RAIS DKT. MWINYI KUANZA ZIARA KATIKA MIKOA MITANO ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajia kuanza ziara ya Kiserikali katiika Mikoa mitano ya Zanzibar kuanzia Julai 16, 2022. Ziara hiyo itaanzia Mkoa wa Mjini Magharibi na kudumu hadi Julai 18, 2022, ambapo Dk. Mwinyi atakagua miradi mbali mbali ya maendeleo hususan ile inayoendelezwa kupitia Fedha za

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajia kuanza ziara ya Kiserikali katiika Mikoa mitano ya Zanzibar kuanzia Julai 16, 2022.

Ziara hiyo itaanzia Mkoa wa Mjini Magharibi na kudumu hadi Julai 18, 2022, ambapo Dk. Mwinyi atakagua miradi mbali mbali ya maendeleo hususan ile inayoendelezwa kupitia Fedha za Uviko -19, ikiwemo miradi ya Maji safi na salama, Afya, elimu pamoja na  barabara katika Wilaya za Mjini Magharibi A’ na ‘B’ ambapo pamoja na shughuli nyengine ataweka  mawe ya msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu Zanzibar, Katibu wa Rais Masoud Balozi alisema ziara hiyo ina lengo la kuangalia utendaji kazi wa miradi ilioanzishwa pamoja na kufuatilia utekelezaji wa ahadi zake wka wananchi.

Alisema kabla ya kuanza ziara ya kukagua miradi hiypo, atapata fursa ya kupokea taarifa za Utekelezaji za Mikoa husika.

Alisema ziara hiyo ya Dk. Mwinyi itaendelea  katika Mkoa wa Kaskazini Unguja mnamo Julai 19, 2022 na kudumu hadi Julai 21, 2022 ambapo atatembeela miradi mbali mbali katika Wilaya ya Kaskazini ‘A’, Kaskazini ‘B’ pamoja na Wilaya Ndogo Tumbatu.

Aidha, alisema ziara hiyo itaendelea Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo katika Wilaya za Kusini na Wilaya Kati Unguja.

Katika hatua nyengine,  alisema  Julai 24,2022 Dk. Mwinyi ataelekea Kisiwani Pemba na kuendelea na ziara hiyo kwa kuanzia na Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo Julai 25,2022 atapata fursa ya kutembelea miradi mbali katika Wilaya za Wete na  Julai 26, 2022 atatembelea Wilaya Micheweni.

Aidha, Julai 27 na 28, 2022  Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi atatembelea Mkoa Kusini Pemba.

Aliwataka wanadishi hao wa habari kushiriki kikamilifu katika ziara hiyo ili kwajuvya wananchi yale yanayoendelea.  

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »