NAIBU WAZIRI NDEJEMBI AIELEKEZA TASAF KUJENGA UZIO SHULE YA SEKONDARI YA OLDONYOWAS ILI KULINDA MIUNDOMBINU YA SERIKALI

NAIBU WAZIRI  NDEJEMBI AIELEKEZA TASAF KUJENGA UZIO SHULE YA SEKONDARI YA OLDONYOWAS ILI KULINDA MIUNDOMBINU YA SERIKALI

Na Barnabas Kisengi -Arusha. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi ameuelekeza uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kujenga uzio katika Shule ya Sekondari ya Oldonyowas iliyopo katika Kijiji cha Oldonyowas Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, ili kulinda miundombinu ya Serikali iliyojengwa kwa jitihada

Na Barnabas Kisengi -Arusha.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi ameuelekeza uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kujenga uzio katika Shule ya Sekondari ya Oldonyowas iliyopo katika Kijiji cha Oldonyowas Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, ili kulinda miundombinu ya Serikali iliyojengwa kwa jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni pamoja na kuimarisha usalama wa wanafunzi wa shule hiyo.


Ndejembi ametoa maelekezo hayo, mara baada ya kukagua mabweni mawili ya wanafunzi wa kiume katika shule ya Sekondari Oldonyowas, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
“TASAF oneni ni kwa namna gani mtawezesha kwa haraka ujenzi wa uzio wa shule ya Sekondari ya Oldonyowas ili kuboresha usalama wa wanafunzi na kulinda miundombinu ambayo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ametumia fedha nyingi za UVIKO katika kujenga mabweni ya wanafunzi wa kike na kiume pamoja na madarasa,” Amesisitiza Ndejembi.


Kwa upande wake, mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Oldonyowas, Bi. Cecilia Sarakikya amesema ameupokea kwa mikono miwili mradi wa ujenzi wa mabweni kwasasabu utawasaidia watoto wao kupata sehemu ya kuishi katika mazingira ya shule, ikizingatiwa kuwa familia nyingi za wanafunzi wa shule hiyo ni za wafugaji ambao wanaishi pembezoni, hivyo kuwalazimu wanafunzi kutembea umbali mrefu ili kuhudhuria masomo.


Naye, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Oscar Maduhu ameitaka kamati ya ujenzi kuhakikisha ujenzi wa mabweni unakamilika kwa kiwango kinachostahili.Sanjari na hilo, Bw. Maduhu amewataka wananchi wa Kijiji cha Oldonyowas kuyatunza mabweni hayo pindi yatakapokamilika, ili yawe na manufaa katika kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu kwa watoto wa Kijiji hicho.
Mradi wa ujenzi wa mabweni mawili katika Kijiji cha Oldonyowas unaoendelea kukamilishwa, umefadhiliwa na OPEC kwa uratibu wa TASAF.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »