DUWASA YAWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUUNGANISHIWA MAJI

DUWASA YAWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUUNGANISHIWA MAJI

Na Barnabas Kisengi-Dodoma MKUU wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja kutoka  Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Pendo Mkali amewataka wananchi wa Ntyuka kujitokeza kwa wingi kuomba kuunganishiwa maji kutokana na Mradi unaotekelezwa kwa fedha za Maendeleo ya Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 kukamilika. Amesema hayo  katika kikao cha

Na Barnabas Kisengi-Dodoma


MKUU wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja kutoka  Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Pendo Mkali amewataka wananchi wa Ntyuka kujitokeza kwa wingi kuomba kuunganishiwa maji kutokana na Mradi unaotekelezwa kwa fedha za Maendeleo ya Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 kukamilika.


Amesema hayo  katika kikao cha wananchi wa Kata ya Ntyuka eneo la Ntyuka jijini Dodoma juu ya mradi mkubwa wa kusambaza huduma ya Maji safi na salama.


Bi Pendo Mkalia amesema DUWASA kwa kushirikiana na Benki ya Equity inamuwezesha mwananchi kuunganishiwa maji kwa kupitia mkopo unaotolewa na benki hiyo.

Naye Meneja Biashara kutoka Benki ya Equity, Richard Mwambuluma  amesema mwananchi anatakiwa kufika ofisi za DUWASA na kuomba maunganisho mapya ambapo atapewa gharama zote za maunganisho na kuipeleka benki ili kumuwezesha kupata mkopo atakao lipa ndani ya miezi sita.
Mwambula Ameongeza kuwa mkopo huo ni wa masharti nafuu ambao kila mwananchi mwenye kipato cha kawaida anaweza kuumudu mkopo huo.


Kwa upande wake Mhandisi wa Mradi, Mhandisi James Lyoba amesema mpaka sasa hakuna mwananchi hata mmoja aliyejitokeza kuomba kuunganishiwa licha ya tanki lenye ujazo wa lita 200000 kujaa.


Diwani wa Kata ya Ntyuka, Yona Mkobolaa amesema DUWASA imejipanga sawa sawa katika kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan ndio maana wakaungana na benki ya Equity ili kuweza kuwasaidia wananchi kuunganisha maji na kuwataka kufika ofisi za DUWASA kuomba maji.


Aidha Mkobolaa Amewataka Wananchi wa kata yake ya Ntyuka kuhakisha wanajitokeza kwa wingi kwenda duwasa hukakikisha wanaunganishiwa huduma ya maji katika nyumba zao.
“Napenda niwaambie Wananchi wa kata yangu tumieni hii fursa tuliyopata ya kuunganishiwa maji hata kama hauna pesa Cash ndio maana benk ya Eguty wamejitolea kuwasaidia wananchi ambao hawana hela kwa sasa benk itakukopesha kwa riba nafuu ambayo utakuwa unalipa kidogo kidogo ili kila mwananchi aweze kupata huduma ya Maji Safi na salama kwa sasa”Alisisitiza Mkobolaa


Diwani Mkobolaa amesema kupatikanika kwa huduma ya Maji katika kata yake ya Ntyuka kumekuwa mkombozi mkubwa wa kumtuma mama ndoo kichwani kutokana na kukosa huduma hiyo kwa muda mrefu katika kata yake.
“Wananchi wangu wameteseka sana kwa kutafuta maji kwenye bwawa la mkalama na wakati mwingine kulisababisha ndoa kuvunjika, wasichana kubakwa kutokana na umbali waliokuwa wakitembea kwenda kutafuta huduma ya Maji lakini kwa Sasa niwapongeze Duwasa kwa kazi nzuri mliyoifanya ya kutuletea huduma hii ya Maji kwa ukaribu kabisa sasa hapa Wananchi wangu watakuwa wakioga hata mara kumi kwa siku tafauti na zamani”Alisisitiza Diwani Mkobolaa
Diwani Mkobolaa Amewataka Wananchi wa Ntyuka Sasa kuhakisha wanakuwa walinzi wazuri wa kulinda miundombinu ya mabomba ya Maji yaliyotandazwa kwenye kata yake ya Ntyuka.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »