WAZIRI AWESO AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI CHAMWINO

WAZIRI AWESO AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI CHAMWINO

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji katika Kata ya Dabalo Wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma ambapo ametoa pongezi nyingi Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) na kwa kampuni ya PLASCO inayotengenenza matanki makubwa ya plastiki yaliyotumiwa katika mradi huo ikiwa ni kwa mara ya

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji katika Kata ya Dabalo Wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma ambapo ametoa pongezi nyingi Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) na kwa kampuni ya PLASCO inayotengenenza matanki makubwa ya plastiki yaliyotumiwa katika mradi huo ikiwa ni kwa mara ya kwanza inatumika katika miradi ya maji nchini huku Waziri Aweso akiahidi kuwa Serikali itaendelea kutumia teknolojia hiyo badala ya ya ile ya kujenga kwani inatumia muda mfupi wa wiki mbili tu kuyaweka katika chanzo cha maji  na yanadumu kwa muda mrefu wa zaidi ya miaka 70.


Mradi huo unaogharimu zaidi ya shilingi milioni 907  unatekelezwa na   RUWASA chini ya Ofisi ya Meneja wa Mkoa wa Dodoma na Wilaya ya Chamwino kwa fedha za Mfuko wa Taifa wa Maji ambapo mkandarasi anayeujenga ni Medes Company Limited na unatarajiwa kuhudumia wakazi 8,134 utakapomilika Julai 30, 2022.


Waziri AWESSO amesema mradi huo ukikamilika utawanufaisha Wananchi wengi na amewataka wananchi kutoa ushirikiano mkubwa wakati ujenzi wa mradi huu ukiendelea huku akimtaka Mkandarasi wa mradi huo kuhakisha anafanya kazi kwa juhudi na uzalendo mkubwa na kukamilisha kwa wakati kama mkataba wao unavyoonyesha.


“Nakuelemeza Mkandarasi wa mradi huu fedha ya miradi ya maji haichezewi kabisa nakwambia hakikisha m atekeleza mradi kwa wakati na kiwango maana mradi huu ni wa fedha nyingi na fedha hizi hazichezewi ovyo”Alisisitiza Waziri AWESSO.


Kwaupande wake Mbunge wa Jimbo la Chamwino ambaye pia ni Naibu waziri ofisi ya Rais Mejenimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratus Ndejembi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh RAIS SAMIA SULUH HASSAN kwa kuwajali wana Chamwino kwa kuwapatia mradi mkubwa ambao itawaraisishia wananchi wa Jimboni kwake.
“Nawaomba Wananchi wa Jimbo langu la Chamwino tumepewa mradi huu wenye fedha nyingi hivyo tuhakikishe tunaulinda na kuutunza vizuri mnajua wenyewe shida tuliyokuwa tumaipata hapa sasa Serikali imetuona hivyo ni kuhakikisha tuna tunza miundombinu hii kwa manufaa yetu na vizazi vijavyo”Alisisitiza Ndejembi

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »