DC SHEKIMWERI AWATAKA WAKAZI WA DODOMA KUJITOKEZA KUJIFUNZA UFUGAJI WA KISASA MAADHIMISHO YA NANENANE

DC SHEKIMWERI AWATAKA WAKAZI WA DODOMA KUJITOKEZA KUJIFUNZA UFUGAJI WA KISASA MAADHIMISHO YA NANENANE

Na Barnabas Kisengi , Dodoma Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini JABIR SHEKIMWERI amewataka wananchi wa Wilaya ya Dodoma mjini kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya sherehe za wakulima nanenane zitakazo fanyika jijini dodoma katika viwanja vya nane nane vilivyo nzuguni jijini Domama. SHEKIMWERI ameyasema hayo wakati akizungumza na JFIVE BLOG (jfivetv.com) katika mahojiano maalumu

Na Barnabas Kisengi , Dodoma


Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini JABIR SHEKIMWERI amewataka wananchi wa Wilaya ya Dodoma mjini kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya sherehe za wakulima nanenane zitakazo fanyika jijini dodoma katika viwanja vya nane nane vilivyo nzuguni jijini Domama.


SHEKIMWERI ameyasema hayo wakati akizungumza na JFIVE BLOG (jfivetv.com) katika mahojiano maalumu Ofisini kwake kuelekea kwenye maadhimisho ya sherehe za wakulima nanenane ambopo kanda ya kati zitafanyika jijini Dodoma kwa kushirikiana Mkoa wa Dodoma na singida.
“Sherehe hizi ni fursa kubwa kwa Wananchi wa Mkoa wa dodoma na singida na mikoa ya jirani tunawakaribisha wote waje kujifunza kilimo cha zabuni ambayo inalimwa Mara mbili kwa mwaka na ni zao la kimkakati katika wilaya na mkoa Wetu”amesisitiza Shekimweri.


Aidha Mkuu wa Wilaya amesema Wananchi wajitokeze kwa wingi kujifunza ufugaji wa kuku,mbuzi,ngombe, na ukamuaji wa mafuta ya alizeti ambapo elimu hii wataipata katika mabanda mbalimbali ya maonyesho katika viwanja vya nane nane vilivyo nzuguni jijini Dodoma.
SHEKIMWERI Amewataka Wananchi kuhakisha ifikapo Agost 23 Mwaka huu wajitokeze kwa wingi kushiriki zoezi la sensa ya watu na Makazi.
Kwa upande Wake Afisa Mahusiano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi SARAH MSIKA amesema sherehe za maadhimisho ya sikukuu ya wakulima zitaanza Julai 30 na zitaendelea kufanyika hadi Agost 10  Katika viwanja vya nane nane vilivyo nzuguni jijini Dodoma.


Bi SARAH MSIKA amesema Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Atony Mtaka atashirikia na Mkuu wa Mkoa wa Singida katika sherehe za maadhimisho ya sikukuu ya wakulima nanenane.


Aidha afisa mahusiano amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi huku akiwataka Waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kuandika store mbalimbali na kutengeneza makala ya vipindi mbalimbali katika viwanja vya nane nane vilivyo nzuguni ili kuweza kuutangaza Mkoa wa Dodoma na Singida ambayo ni maarufu kwa kulima zabibu na kilimo cha alizeti na ufugaji wa kuku wa asili.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »