MAKADA WA CCM 48 WAJITOKEZA KUWANIA UBUNGE WA AFRIKA MASHARIKI

MAKADA WA CCM 48 WAJITOKEZA KUWANIA UBUNGE WA AFRIKA MASHARIKI

Na Barnabas Kisengi-Dodoma Zoezi la Uchukuaji wa fomu za kuwania Ubunge wa Afika Mashariki linaendelea tangu lianze Agost 1, 2022 katika ofisi tatu za chama cha Mapinduzi Ofisi ya Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoani Dodoma, Ofisi ndogo Lumumba Dar es Salaam na Afisi kuu Zanzibar. Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za

Na Barnabas Kisengi-Dodoma


Zoezi la Uchukuaji wa fomu za kuwania Ubunge wa Afika Mashariki linaendelea tangu lianze Agost 1, 2022 katika ofisi tatu za chama cha Mapinduzi Ofisi ya Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoani Dodoma, Ofisi ndogo Lumumba Dar es Salaam na Afisi kuu Zanzibar.


Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama cha Mapinduzi Makao Makuu Katibu wa Halimashauri kuu ya CCM Organazesheni Maudline Castico Amesema hadi leo Agosti 03,  2022 jumla ya wagombea 48 wamekwisha kuchukua fomu na kurusha katika ofisi za Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoani Dodoma, Ofisi ndogo Lumumba Dar es Salaam na Afisi kuu Zanzibar.


Aidha Katibu wa Halimashauri kuu ya CCM Organazesheni Maudline Castico amesema fomu hizo za kuwania Ubunge wa Afika Mashariki linaendelea hadi Tarehe 10 Agost 2022 ndio mwisho wa kuchukua fomu hizo.


Bi Maudline Castico amesema wanachama wote wa chama cha Mapinduzi hapa nchi ambaye anaona anasifa za kuchukua fomu milango iko wazi anamwakilisha ili waweze kwenda kuwania nafasi hizo za Ubunge wa Afika Mashariki.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »