MANARA, ENG. HERSI WASHTAKIWA TFF

MANARA, ENG. HERSI WASHTAKIWA TFF

Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungulia mashtaka ya kimaadili Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said na aliyekuwa ofisa wa klabu hiyo Haji Manara. Kamati ya Maadili ya TFF hivi karibuni ilimfungia miaka miwili Manara kujihusisha na shughuli yoyote ya mpira wa miguu (any football-related activity), lakini ameshindwa kutekeleza adhabu hiyo. Naye

Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungulia mashtaka ya kimaadili Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said na aliyekuwa ofisa wa klabu hiyo Haji Manara.

Kamati ya Maadili ya TFF hivi karibuni ilimfungia miaka miwili Manara kujihusisha na shughuli yoyote ya mpira wa miguu (any football-related activity), lakini ameshindwa kutekeleza adhabu hiyo.

Naye Mhandisi Said amefunguliwa mashtaka kwa kwenda kinyume na Ibara ya 16(1)(a) ya Katiba ya TFF, pamoja na Ibara ya 1(6) ya Katiba ya Yanga.

Baada ya Manara kuadhibiwa na Kamati ya Maadili ya TFF, Sekretarieti ilimwandikia barua Mhandisi Said kuhakikisha klabu yake inaheshimu uamuzi huo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya TFF tayari amepelekewa mashtaka hayo, walalamikiwa watapewa mashtaka na mwito mara baada ya Kamati hiyo kupanga tarehe ya kusikiliza mashtaka hayo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »