UWT TAWI LA CHINYOYO JIJINI DODOMA WAPATA VIONGOZI WAPYA

UWT TAWI LA CHINYOYO JIJINI DODOMA WAPATA VIONGOZI WAPYA

Na Barnabas Kisengi-Dodoma. Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tawi la chinyoyo kata ya kilimani Jijini Dodoma (U.W.T) wamefanya Uchaguzi wa viongozi wa ngazi mbalimbali katika Jumuiya hiyo na kupata viongozi watakaongoza jumuiya hiyo ya Tawi la chinyoya kwa kipindi cha miaka mitano. Uchaguzi huo ulikuwa katika kuwania nafasi  mbalimbali za Jumuiya

Na Barnabas Kisengi-Dodoma.


Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tawi la chinyoyo kata ya kilimani Jijini Dodoma (U.W.T) wamefanya Uchaguzi wa viongozi wa ngazi mbalimbali katika Jumuiya hiyo na kupata viongozi watakaongoza jumuiya hiyo ya Tawi la chinyoya kwa kipindi cha miaka mitano.


Uchaguzi huo ulikuwa katika kuwania nafasi  mbalimbali za Jumuiya ya umoja wa Wanawake Tawi la chinyoyo akisoma matokeo ya uchaguzi huo Mwenyekiti wa wa Umoja wa Vijana kata ya kilimani ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani Ndugu ALLY YUNUS amesema wajumbe halali wa jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tawi la chinyoyo (UWT) walio piga kura walikuwa 102.


Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Mwenyekiti Mjumbe wa kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani Ndugu ALLY YUNUS amesema katika nafasi ya uwakilishi kamati ya Utekelezaji Tawi nafasi zilikuwa sita na wagombea walikuwa saba walio shinda ni Erika chamsingo kura 77. Egla Mgosi kura 76, Frola Iboko Kura 76, Marietha Ndimbo kura 74, Evelina Assa kura 72 na Cathelin Mwakasanga kura 56.


Katika nafasi ya Mjumbe wa mkutano Mkuu wa kata nafasi zilikuwa mbili na wagombea walikuwa watano walioshinda ni Cathelin Mwakasanga kura 46 na Magreth Milambo kura kura 54 na katika nafasi ya Halimashauri kuu ya Tawi nafasi ilikuwa moja na mgombea alikuwa moja hivyo alipigiwa kura za ndiyo na hapana mgombea alikuwa Jane Mwangosi kura za hapana zilikuwa 31 na kura za ndiyo zilikuwa 59 hivyo Jane Mwangosi amepita katika nafasi hiyo ya mkutano Mkuu wa kata.


Aidha Ndugu ALLY YUNUS ameendelea kutangaza nafasi nyingine ni uwakilishi wazazi nafasi ilikuwa moja na mgombea alikuwa moja Emmaleceana komba alipigiwa kura za ndiyo na hapana ambapa kura za hapana zilikuwa 37 na kura za ndiyo zilikuwa 58 hivyo namtangaza Emmaleceana komba amepita katika nafasi hiyo pia katika nafasi ya Mjumbe wa UWT kupita uwakilishi wa Vijana nafasi ilikuwa moja na wagombea walikuwa wawili Victoria Wanyange amepata kura 41  na Veronica Chikoti amepata kura 55 hivyo namtangaza Veronica Chikoti amepita katika nafasi hiyo.


Ndugu ALLY YUNUS ameendelea kusema nafasi nyingine ni nafasi muhimu sana Katika jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tawi la chinyoyo (UWT) ni nafasi ya katibu wa UWT Tawi nafasi ilikuwa moja na mgombea walikuwa wawili Domina Kiria amepata kura 53 na Joyce Mnyanika amepata Kura 43 hivyo namtangaza Domina Kiria kuwa katibu wa UWT Tawi la chinyoyo.


Ndugu ALLY YUNUS ameendelea kumaliza kutangaza nafasi muhimu ya Mwenyekiti wa UWT Tawi la chinyoyo ambapo nafasi ilikuwa moja na wagombea walikuwa watu Anne Zebedayo amepata kura 55,  Flora Chogelo amepata kura 3 na Raha Mpela amepata kura 41 hivyo kwa mamlaka niliyopewa ninamtangaza Ndugu ANNE ZEBEDAYO kuwa ndiye Mwenyekiti wa wa jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tawi la chinyoyo.


Uchaguzi huo umefanyika baada ya Uchaguzi wa kwanza kufutwa na uongozi wa ngazi ya Wilaya Kwa kutotimiza vigezo mbalimbali na sasa kurudiwa na kuwapata viongozi hao watakao iongoza jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tawi la chinyoyo (YET)
Uchaguzi huo wa jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tawi la chinyoyo (UWT) ulisimamiwa na wasimamizi walio teuli na halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani ambao ni wajumbe wa kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani Ndugu ALLY YUNUS, Barnabas Kisengi na Tatu Rashidi kwa kushirikiana na katibu wa jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) wilaya ya Dodoma Mjini ambapo Uchaguzi huo ilifanyika vizuri na wagombea wote waliridhika na matokeo yao na kukubali kusaini matokeo yao.


Ikumbwukwe Chama cha Mapinduzi hivi sasa linaendelea na chaguzi zake mbalimbali zilizo anzia nganzi za mashina,matawi, kata, wilaya, Mkoa hadi Taifa ili kuweza kuwapata viongozi mbalimbali watakao kiongoza Chama cha Mapinduzi katika nafasi mbalimbali kwa miaka mitano.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »