MKUU WA WILAYA YA IRAMBA AANZISHA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU KUWAKUTANISHA PAMOJA VIJANA

MKUU WA WILAYA YA IRAMBA AANZISHA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU KUWAKUTANISHA PAMOJA VIJANA

Na Mwandishi Wetu Iramba Singida Ili kuwakutanisha vijana pamoja kwa ajili ya kuimarisha afya zao, kutambua vipaji na kuviendeleza Wilaya ya Iramba imejipanga kuanza mashindano ya mpira miguu. Mashindano hayo yanayoratibiwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Mwenda yanatarajiwa kuanza mapema mara baada ya msimu wa kilimo kumalizika. Mkuu wa Wilaya  Mwenda

Na Mwandishi Wetu Iramba Singida


Ili kuwakutanisha vijana pamoja kwa ajili ya kuimarisha afya zao, kutambua vipaji na kuviendeleza Wilaya ya Iramba imejipanga kuanza mashindano ya mpira miguu.


Mashindano hayo yanayoratibiwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Mwenda yanatarajiwa kuanza mapema mara baada ya msimu wa kilimo kumalizika.


Mkuu wa Wilaya  Mwenda amebainisha hayo Januari, 13, 2023 wakati akizingumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya WazoHuru Media Group Limited Ndg Mathias Canal aliyemtembelea ofisini kwake Mjini Kiomboi.


Mwenda amesema kuwa Ligi ya mpira wa miguu ambayo ina lengo la kuimarisha sekta ya michezo Wilayani hapo na kuwakutanisha vijana itasaidia kutengeneza mahusiano imara na madhubuti katika msingi wa maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na Wilaya kwa ujumla wake.


Mkuu wa Wilaya ya Iramba  amewasihi wananchi na wadhamini mbalimbali kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha dhamira hiyo katika kuimarisha sekta ya michezo na kufanikisha kuanza na kumalizika kwa mashindano hayo.


Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya WazoHuru Media Group Limited Ndg Mathias Canal amempongeza DC MWENDA kwa kujipanga kuanzisha mashindano hayo ambayo yatakuwa chachu ya kuitangaza Wilaya ya Iramba na sekta ya uwekezaji.
Amesema kuwa Wilaya ya Iramba ina maeneo mengi mazuri na ardhi ya kutosha kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya Kilimo, Elimu, Mifugo na Uvuvi ikiwa ni pamoja na sekta ya Viwanda.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »