WCF kuwahakikishia kipato Wafanyakazi wanaopata ulemavu wa kudumu

WCF kuwahakikishia kipato Wafanyakazi wanaopata ulemavu wa kudumu

Na Moree Rojas Dodoma. WCF ni mdau muhimu katika kupunguza umasikini kwenye taifa kwa kuwahakikishia kipato wafanyakazi wanaopata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali au magonjwa yatokanayo na kazi. Dkt.John Mduma Mkurugenzi Mkuu WCF amesema hayo  wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma  kueleza utekelezaji wa majukumu ya mfuko wa fidia kwa wafanyakazi katika

Na Moree Rojas Dodoma.


WCF ni mdau muhimu katika kupunguza umasikini kwenye taifa kwa kuwahakikishia kipato wafanyakazi wanaopata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali au magonjwa yatokanayo na kazi.


Dkt.John Mduma Mkurugenzi Mkuu WCF amesema hayo  wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma  kueleza utekelezaji wa majukumu ya mfuko wa fidia kwa wafanyakazi katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita.


Aidha amesema kabla ya kuanzishwa kwa mfuko huo wa WCF wafanyakazi wa sekta binafsi waliopata ulemavu walikuwa wakilipwa kwa mkupuo kiasi cha shilingi 108,000 tu na wafanyakazi wa sekta ya umma waliopata ulemavu wa kudumu walikuwa wakilipwa kwa mkupuo kiasi cha shilingi milioni 12 tu bila kujali kama ulemavu huo umewapotezea kabisa uwezo wa kufanya kazi na kupata kipato.
“Mfuko umekuwa ukilipa fidia kwa mfumo wa pensheni ya kila mwezi kwa wategemezi au wafanyakazi waliopata ulemavu unaozidi asilimia 30 inayofikia hadi asilimia 70 ya mshahara wa wafanyakazi jambo linalomwezesha mfanyakazi au wategemezi wao kuepukana na umaskini” Amesema Dkt.Mduma


Aidha Dkt Mduma amesema WCF inasaidia katika kuongeza tija katika uzalishaji kwa kuwapa fursa waajiri kujikita katika uzalishaji na kupunguza migogoro ya kazi inayotokana na fidia kwa wafanyakazi.
“Kimsingi WCF inalenga kuhakikisha kuwa nguvu kazi ya taifa inalindwa,jukumu hili linatekelezwa kwa kuwahudumia wafanyakazi wanaoumia au kuugua kazini kwa lengo la kuwarejesha kazini haraka iwezekanavyo jukumu hili linatekelezwa kupitia uhamasishaji wa mbinu za kuzuia ajali na magonjwa yatokanayo na kazi”Amesisitiza Dkt Mduma


Mkurugenzi Mkuu WCF  amesema Ibara ya 11 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inaitaka serikali kuweka utaratibu wa kupata msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzee maradhi au hali ya ulemavu katika hali nyinginezo za mtu kuwa hajiwezi.
“Uwepo wa WCF taifa linakuwa limetimiza wajibu wake wa kikatiba wa kuwalinda wafanyakazi dhidi ya madhara yatokanayo na ulemavu wa kudumu”amesema Dkt Mduma


Taifa lianakuwa limetimiza matakwa ya mikataba ya kimataifa ambayo ni pamoja na mikataba ya shirika la kazi duniani(ILO Conventions) na 017,102 na 121.
Hadi kufikia  June. 30  2022 WCF imesajili jumla ya waajiri 27,786 ikiwa ni asilimia 90 ya waajiri 30,846 walioko kwenye kanzidata ya mfuko.
Mfuko ulianza rasmi kukusanya michango kwa waajiri kuanzia  Julai 01  2015 hadi kufikwa  Juni. 30 2022 makusanyo ya jumla ya michango yalifikia shilingi bilioni 545.49.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »