EURO MILIONI 9 KUTUMIKA KUTEKELEZA MRADI WA MATUMIZI BORA YA NISHATI

EURO MILIONI 9 KUTUMIKA KUTEKELEZA MRADI WA MATUMIZI BORA YA NISHATI

Na Moreen Rojas Dodoma. Euro milioni 9 kutumika kutekeleza matumizi bora ya nishati ambapo Euro milioni 8 kutoka jumuiya ya ulaya huku UNDP ambao ni washiriki katika utekelezaji wa mradi huu wakifadhili Euro milioni 1. Hayo yameelezwa na Emilian Nyanda afisa kutoka wizara ya nishati ambaye ni mratibu wa mradi wa utekelezaji wa matumizi bora

Na Moreen Rojas Dodoma.


Euro milioni 9 kutumika kutekeleza matumizi bora ya nishati ambapo Euro milioni 8 kutoka jumuiya ya ulaya huku UNDP ambao ni washiriki katika utekelezaji wa mradi huu wakifadhili Euro milioni 1.


Hayo yameelezwa na Emilian Nyanda afisa kutoka wizara ya nishati ambaye ni mratibu wa mradi wa utekelezaji wa matumizi bora ya nishati.


Aidha amesema mradi huu utasaidia kupunguza matumizi ya nishati yasiyoyalazima pamoja na kupunguza gharama za nishati hata katika utunzaji wa mazingira katika sekta ya nishati.


Wizara ya nishati inajukumu zima la kusimamia matumizi bora ya nishati kwa kushirikiana na sekta mbalimbali ikiwemo Tamisemi,Ewura pamoja na wizara ya ujenzi na uchukuzi ambapo mradi utawasaidia katika kuja na mifumo,miongozo ya matumizi bora ya nishati hususani katika majengo.
“Mlengwa ni mwananchi tunataka kumueleza kutokana na juhudi zote hizi wananchi kuacha kutumia umeme mwingi pasipo ulazima” Amesema Nyanda
Aidha amesema kuwa bado hawajajua vifaa watakavyoanza navyo lakini wanatafuta mshauri ambae atazunguka kwa wadau na serikali kuuliza ni vifaa gani vinatumika sana hapa nchini mfano fridge zinatumika kwa kiwango kikubwa.
“Tulichogundua ni kwamba ili tufanikishe tunahitaji kutoa elimu kwa umma ndio maana tunawatumia waandishi wa habari ili kuwafikia wananchi kwa urahisi na kuchukua hatua stahiki”Amesisitiza Nyanda


Aidha amesema hivi karibuni tumesikia hatua za Waziri wa nishati January Makamba na Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluh Hassan kuhusiana na nishati ya kupikia kuwahamasisha kina mama kutumia nishati mbadala mfano mkaa mbadala ili kutunza mazingira na kuboresha afya ya kina mama,jamii na nchi kwa ujumla.


Aidha miongozo itakayoandaliwa itawaongoza mananchi na kupata elimu kwamba balbu yenye matumizi mazuri ya nishati haitumii umeme mwingi niya kiasi na watu wa TBS watakua wanalifanyia kazi na miongozo itakuja kwamba yeyote anayetengeneza au anayeagiza balbu ziwe za kiwango hiki ili tumsaidie mwananchi.
” Mfano suala la taa wananchi wengi wanalalamika mbona unit za umeme zinaisha haraka kumbe inawezekana vifaa anavyotumia vinatumia umeme mwingi pasipo ulazima”


Kupitia mradi huu kutakuwa na intervention ya vifaa labda vimetengenezwa Tanzania bablu au nyaya vitakuja kwenye viwango kama inakiwango cha matumizi ya chini kwa huduma zilezile.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »