RAIS DK.MWINYI AMEKUTANA NA BALOZI WA UBELGIJI

RAIS DK.MWINYI AMEKUTANA NA BALOZI WA UBELGIJI

Zanzibar,06 Aprili, 2023SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imejikiza zaidi kwenyeteknolojia ya kisasa ili kuboresha sekta ya utalii kwa kuimarishamiundominu ya kisasa ya utoaji huduma bora kupitia viwanja vya ndege vyaZanzibar ili kuwavutia watalii wengi zaidi kutoka mataifa mbambali ya duniawanaoitembelea Zanzibar ili wakirudi kwao wawe mabalozi wazuriwakusimulia mazuri yanayopatikana kwenye visiwa vya Unguja na

Zanzibar,
06 Aprili, 2023
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imejikiza zaidi kwenye
teknolojia ya kisasa ili kuboresha sekta ya utalii kwa kuimarisha
miundominu ya kisasa ya utoaji huduma bora kupitia viwanja vya ndege vya
Zanzibar ili kuwavutia watalii wengi zaidi kutoka mataifa mbambali ya dunia
wanaoitembelea Zanzibar ili wakirudi kwao wawe mabalozi wazuri
wakusimulia mazuri yanayopatikana kwenye visiwa vya Unguja na Pemba na
Tanzaia kwa ujumla.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi
ameyasema hayo alipozungumza na Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Mhe.
Peter Huyghebaert, Ikulu Zanzibar aliefika kujitambulisha.
Dk. Mwinyi, alimueleza balozi huyo kwamba Zanzibar utalii ndio sekta mama ya
uchumi ambao inahusisha na sekta nyengine za uwekezaji kupitia sera yake ya
uchumi wa Buluu.
Rais Mwinyi alisema Uhusiano uliopo baina ya Ubelgiji na Tanzania ikiwemo
Zanzibar kumekuwa na urafiki mzuri baina yao kwani nchi imekuwa ikipokea
watalii wengi kutoka huko.
Alisema kupitia sekta ya utalii kumekuwa na safari za ndege za moja kwa moja
kutoka Ubelgiji hadi Zanzibar na kumueleza balozi huyo uhusiano uliopo baina ya
pande mbili hizo anaamini wataalii zaidi wataongezeka katika kuimarisha urafiki
wao.
“Zanzibar tuna safari za ndege za moja kwa moja kutoka Ubegiji, hali hii pia
imeongeza watalii wengi kutoka huko, tunaamini idadi itaongezeka zaidi kutokana
uhusiano mzuri baina yetu” alisifu, Dk. Mwinyi.
Akizungumzia sekta ya Afya Rais Dk. aliueleza balozi huyo kuangalia uwezekano
wakuimarisha ushirikiano zaidi kwenye sekta hiyo hasa masuala ya TEHAMA
ambako eneo hilo lina uhitaji zaidi ili kuongeza ujuzi na kubadilishana uzoefu kwa
wafanyakazi na wahudumu wa fani hiyo kupitia taasisi ya Karume amako vijana
wengi huchukua fani ya Afya.
Pia Rais Dk. Mwinyi alimueleza Balozi Huyghebaert ikiwa Ubelgiji ni mwanachama
wa Umoja wa Ulaya (EU) yenye miradi mingi ya maendeleo kuangalia zaidi fursa
zilizopo kupitia ushirikiano wa diplomasia uliopo baina ya Ubelgiji na Tanzania
ikiwemo Zanzibar kunufaika na fursa zilizopo huko na uwezekano wa kuzifikia
katika kuimarisha zaidi uhusino baina yao.
Kwa upande wake Bolozi Peter Huyghebaert, aliishurkuru Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar na kumpongera Rais Dk. Mwinyi kwa juhudi zake za kuiletea maendeleo
Zanzibar.
Alisema urafiki wa diplomasia uliopo baina ya Ubelgiji na Tanzania ikiwemo
Zanzibar anaamini utaendelea kuzaa matunda mazuri yatakayowanufaisha
wananchi wa pande mbili hizo.
Alisema Ubelgiji imekua ikishirikiana zaidi na Afika kupitia miradi mbalimbali ya
maendeleo kwa sekta zote za taasisi za umma na binafsi.

Alimueleza Rais Dk. Mwinyi kwamba hadi sasa Ubelgiji inaendeleza miradi
mbalimbali kwenye kanda tano za Afrika, Tanznia ikiwa miongoni mwao kwa
kuyafikia maeneo mengi hasa kwenye sekta mtandao ikiwemo kushirikina katika
masuala ya Afya mtandao ambako Ubekgiji na Tanzania wanashirikiana kwenye
matumizi ya teknolojia ya kisasa kuangalia uwezekano wa kunusuru vifo vya
watoto kabla ya kuzaliwa, aidha, masuala ya huduma za pasi mtandao ambako
Ubelgiji inashirikiana na Idara ya uhamiaji na sekta nyengine kwenye ustawi wa
maendeleo ukiwemo mradi wa “wanawake wanaweza” katika kuwainua wanawake
kuendana na maadiliko chanya ya maendeo na kujikwamua kiuchumi kupitia
taasisi za serikali na asasi za kiraia.
Pia balozi huyo alimuahidi Dk. Mwinyi kushirikiana kwenye maeneo mbalimbali ya
maendeleo ikiwemo kuimarisha matumizi ya IT na teknolojia hasa kwenye sekta
ya afya kwa kuimarisha huduma za Afya mtandao pamoja na kuangalia fursa
zilizopo kupitia uchumi wa buluu jinsi ya kuwanufaisha wananchi wa pande mbili
hizo katika kuendeleza uhusiano wa kirafiki uliopo baina yao.
Tanzania na Ubelgiji zimekua na uhusiano wa diplomasia na biashara tangu
miaka ya 1980 ambapo kwa mara ya kwanza Ubelgiji ilifungua ubalozi wake Dar
es Salaam mwaka huo na Tanzania ilifungua ubalozi wake mji mkuu wa nchi hiyo,
Brussels ambako balozi wa Tanzania nchini humo ni Mhe. Jestas Abouk
Nyamanga tangu mwaka 2019
IDARA YA MAWASILINO, IKULU ZANZIBAR

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »