NAMBA 199 MKOMBOZI KWA WANANCHI KUPATA UFAFANUZI MASUALA YA AFYA

NAMBA 199 MKOMBOZI KWA WANANCHI KUPATA UFAFANUZI MASUALA YA AFYA

Imeelezwa kuwa  Kituo cha Huduma ya Simu cha Wizara   ya Afya  199 (Afya Call Center) kupitia Elimu ya Afya kwa Umma kimekuwa na mchango mkubwa  katika kutatua hoja za wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya afya. Hayo yamesemwa na Beatrice Titho kutoka  Wizara ya Afya,Elimu ya Afya kwa Umma ,  Kituo cha Huduma ya Simu cha

Imeelezwa kuwa  Kituo cha Huduma ya Simu cha Wizara   ya Afya  199 (Afya Call Center) kupitia Elimu ya Afya kwa Umma kimekuwa na mchango mkubwa  katika kutatua hoja za wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya afya.

Hayo yamesemwa na Beatrice Titho kutoka  Wizara ya Afya,Elimu ya Afya kwa Umma ,  Kituo cha Huduma ya Simu cha Wizara(Afya Call Center) katika hitimisho ya mafunzo kwa Watumishi katika Idara/Vitengo/Programu jinsi ya kutumia  mfumo wa taarifa wa Wizara ya Afya  kujibu hoja au tetesi  zinazowasilishwa na wananchi.

Titho amesema kutokana na juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu kuhakikisha huduma bora za afya zinaifika kwa kila jamii wananchi wamekuwa wakipiga namba bure 199 ili kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya afya.

“Kituo hiki kimeweka wananchi karibu na Wizara na kuweza kupewa ufafanuzi mahala walipo kwa kupiga simu namba 199  bure hivyo kupitia mafunzo haya kwa watumishi itaongeza ari katika utendaji wa kazi”amesema Titho.

Kwa upande wake Afisa Muuguzi Mwandamizi kutoka Elimu ya Afya kwa Umma, Mpango wa Taifa wa Huduma za Afya ngazi ya Jamii  Orsolina Tolage amesema mafunzo hayo yamekuwa na mchango mkubwa namna ya kuingia kwenye mfumo na umuhimu wa kufuata miongozo namna ya kumjibu mwananchi pindi anapohitaji ufafanuzi masuala ya afya kupitia namba 199 .

“Nimefaidika sana na mafunzo haya kwani tumepewa uelewa namna gani unaweza kuingia kwenye mfumo na kuona hoja mbalimbali zilizotolewa na  wananchi kupitia Afya Call Center  na umuhimu wa kuzijibu kwa wakati pia umuhimu kushirikishana kwenye idara kwa kufuata miongozo namna gani unamjibu mwananchi”amesema.

Hussein Kilwanila ni Msimamizi Utawala kutoka Programu ya Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele(NTD) amesema namba 199 imesaidia kwa kiwango kikubwa kwa wananchi kuomba ufafanuzi.

“Mwanzoni kabla ya namba 199 wakati mwingine mpaka uende katika kituo cha afya kilichokaribu na unatumia muda mrefu lakini namba hii tuna ushuhuda mtu anapiga simu mahala popote anapata ufafanuzi wa afya afanye nini hivyo katika programu yetu Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele imetusaidia sana”amesema Kilwanila.

Kwa upande wake Penford Joel kutoka Elimu ya Afya kwa Umma amesema  kutokana na serikali kuelekeza jitihada za utoaji wa elimu namba 199 inamsaidia mtu mahala popote kupiga simu na kupata ufafanuzi hivyo kupitia mafunzo hayo yana mchango mkubwa kwa watumishi.

Ikumbukwe kuwa Mafunzo kwa Watumishi katika Idara/Vitengo/Programu jinsi ya kutumia  mfumo wa taarifa wa Wizara ya Afya  kujibu hoja au tetesi  zinazowasilishwa na wananchi yamedumu kwa siku mbili na yameratibiwa na Wizara ya Afya, Idara ya Kinga Elimu ya Afya kwa Umma kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani(UNICEF).

MWISHO.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »