Madaktari Bingwa husaidia Kupunguza Foleni Hospitali za Mikoa.

Madaktari Bingwa husaidia Kupunguza Foleni Hospitali za Mikoa.

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ujiji kilichopo mkoani Kigoma, Dkt. Edwin Muchunguzi amesema kuwa ujuzi na mafunzo yanayoendelea kutolewa na Madaktari Bingwa waliosambazwa katika baadhi ya vituo vya afya nchini kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi wa vituo hivyo katika eneo la huduma ya mama na mtoto, yatasaidia kupunguza foleni ya wakina mama na

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ujiji kilichopo mkoani Kigoma, Dkt. Edwin Muchunguzi amesema kuwa ujuzi na mafunzo yanayoendelea kutolewa na Madaktari Bingwa waliosambazwa katika baadhi ya vituo vya afya nchini kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi wa vituo hivyo katika eneo la huduma ya mama na mtoto, yatasaidia kupunguza foleni ya wakina mama na watoto kutibiwa katika hospitali za Mikoa kwani huduma nyingi zitakuwa zikitolewa katika vituo hivyo.

Dkt. Muchunguzi ameyasema hayo hivi karibuni wakati akihojiwa na Waandishi wa Habari juu ya umuhimu wa mafunzo yanayotolewa na timu ya wataalam wa afya wakiwemo Madaktari Bingwa wa Wakina Mama na Uzazi, Madaktari Bingwa wa Watoto, Madaktari Bingwa wa Dawa za Usingizi na Ganzi na Wakunga Wabobezi nchini waliopelekwa na Wizara ya Afya chini ya Kampeni inayojulikana kama ‘Madaktari wa Mama Samia’ inayoratibiwa na wizara hiyo.

“Huduma za mama na mtoto zilizokuwa zikitolewa katika vituo vya afya vingi ni za uzazi wa kawaida na upasuaji wa kawaida lakini baada ya wataalam hawa kutuongezea ujuzi wa kutatua baadhi ya changamoto zingine za uzazi zilizokuwa zinashindikana, hakuna haja tena kwa wanawake hawa kujazana kwenye hospitali ya Mkoa na badala yake huduma watazipata hapa hapa kituoni”, alisema Dkt. Muchunguzi.

Vilevile, ameendelea kumshukuru Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kuleta programu hiyo katika vituo vya awali vya kutolea huduma ambapo wakina mama takriban 300 hadi 400 wanajifungulia kwenye vituo hivyo kila mwezi na kuongeza kuwa programu hiyo ni ya muhimu kutolewa ili kusaidia kutokomeza kabisa vifo vya mama na mtoto kama lilivyo lengo la Wizara ya afya.

“Pongezi nyingi ziende kwa Wizara ya Afya kwani ujio wa Madaktari Bingwa na Wakunga Wabobezi umeleta matokeo chanya katika utoaji wa huduma za mama na mtoto katika kituo chetu cha afya cha Ujiji”, aliongeza Dkt. Muchunguzi.

Aidha. Dkt. Muchunguzi ametoa rai kwa watumishi wengine wa afya kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwani kada hiyo ipo kwa lengo la kuhudumia wananchi na ili kuendelea kuokoa maisha ya wengi hasa wanawake na watoto inatakiwa kujitoa kwa hali zote.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Masuala ya Usingizi na Ganzi ambaye ni mmoja wa Wakufunzi wa Watumishi wa Kituo hicho, Dkt. Allen Kitalu amesema kuwa wamewawezesha wafanyakazi wa kituo hicho katika utoaji wa dawa za usingizi na namna ya kupambana na changamoto mbalimbali zinazotokea katika utoaji wa dawa za usingizi.

“Kwa Tanzania bado tuko nyuma kidogo katika suala zima la utoaji wa dawa za usingizi katika vituo vyetu vya afya kwa hiyo, tumefika hapa ili kuwawezesha wataalam waliopo waweze kutoa huduma hii kwa viwango na ubora unaotakiwa, mpaka sasa hivi tumeweza kuwajengea uwezo na kuwafikisha katika kiwango ambacho wanaweza kutoa dawa za usingizi kwa viwango na usalama wa hali ya juu, alisema Dkt. Kitalu.
Picha ya kwanza: Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ujiji kilichopo mkoani Kigoma, Dkt. Edwin Muchunguzi akizungumza na Maafisa Habari wa Idara ya Habari – MAELEZO hivi karibuni kuhusu ujio wa Madaktari Bingwa wa Mama waliosambazwa na Wizara ya Afya kwa ajili ya kutoa mafunzo ya afya ya mama na mtoto kwa wahudumu wa vituo vya afya.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Translate »