ILEMBO YAJIPANGA KUENDELEZA UBINGWA.

ILEMBO YAJIPANGA KUENDELEZA UBINGWA.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mpanda iliyopo mkoani Katavi, Dkt. Paul Swakala amesema anatarajia baada ya watumishi wa afya wa kituo cha Ilembo kupata mafunzo, ubingwa na uwezo kutoka kwa Madaktari Bingwa walioletwa na Serikali kituoni hapo, ataweka mikakati ya kuendeleza ubingwa watakaoachiwa ambapo mbali na mafunzo, yapo mambo mengi ambayo wameyaweka sawa ikiwemo namna

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mpanda iliyopo mkoani Katavi, Dkt. Paul Swakala amesema anatarajia baada ya watumishi wa afya wa kituo cha Ilembo kupata mafunzo, ubingwa na uwezo kutoka kwa Madaktari Bingwa walioletwa na Serikali kituoni hapo, ataweka mikakati ya kuendeleza ubingwa watakaoachiwa ambapo mbali na mafunzo, yapo mambo mengi ambayo wameyaweka sawa ikiwemo namna ya kujipanga kutoa huduma na kufanya upasuaji.

Ameongeza kuwa, yapo mapungufu ambayo yalikuwepo tangu awali lakini tangu wamekuja Madaktari bingwa wa Mama, mengi wameyarekebisha na kuhakikisha kituo hicho kinapiga hatua kubwa katika kuzuia vifo vya mama na mtoto na mwisho wa siku kwa sababu mimba sio ugonjwa asifariki mama hata mmoja.

“Kwa sababu upatikanaji wa Madaktari Bingwa unahitaji muda mrefu, kwa maono yake Rais Samia ameamua kutengeneza mpango maalum wa kuwasambaza Madaktari hawa ili kuboresha miundombinu na mazingira na kufundisha watoa huduma pamoja na kushiriki kwa vitendo kuwahudumia wajawazito na watoto”, alisema Swakala.

“Katika mikakati ya kuendeleza ubingwa tutakaoachiwa, kwanza tutatumia mapungufu yetu yaliyokuwa yanajitokeza ili yatusaidie kwa kuhakikisha kwamba tunayasimamia, kuyaboresha na tutaenenda kulingana na kile ambacho Madaktari Bingwa wametuelekeza kufanya”, aliongeza Dkt. Swakala.

Aidha amefafanua kuwa, juhudi za Serikali na watumishi wa afya zimesaidia kupunguza vifo vya kinamama mathalan kwa Manispaa ya Mpanda kuanzia Januari mpaka Juni, 2023 kati ya wakinamama takriban  2,000 waliojifungua, vifo vilivyotokea ni vitano ambapo kifo kimoja tu ndio kimetoka katika Kituo cha Afya Ilembo.

Ameelezea kuwa, kupungua kwa vifo vya mama na mtoto kumechangiwa na moyo wa Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameamua kuwekeza moyo wake kwa mama na mtoto ambapo ameelekeza juhudi mbalimbali ikiwemo hii ya kusambaza Madaktari Bingwa 100 katika baadhi ya Vituo vya Afya nchini ili kutoa ujuzi walionao kusaidia kuimarisha huduma ya mama na mtoto nchini.

Vilevile, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake ambaye pia ni kiongozi wa timu ya Madaktari Bingwa waliopelekwa katika kituo hicho, Shedrack Magambo ameishukuru Wizara ya Afya kwa kuweza kubuni suala hili linalosaidia kusogeza huduma za kibingwa za mama na mtoto ambapo timu ya watu watano wakiwemo Madaktari na Wauguzi imeweza kutoa huduma na kuwezesha mafunzo kwa watumishi wa Kituo cha Afya cha Ilembo ambao wameonesha kiu kubwa ya kujifunza zaidi.

“Naishukuru Serikali kupitaia Wizara kwa kuviona vituo hivi vinavyohudumia wanawake wengi wajawazito na kuvifanya viwe vya kwanza kupelekewa huduma ya Madaktari Bingwa, hii imesaidia wahudumu wanaohudumia vituo vyenye wamama wengi wanaohitaji kujifungua kupata mafunzo mapema na hivyo kuokoa maisha ya wazazi na watoto wengi watakaohudumiwa katika vituo hivyo”, alisema Dkt. Magambo.

Ameongeza kuwa, Serikali imejenga vituo na imeleta vifaa lakini changamoto inabaki kwenye wataalam na utaalam hivyo uwepo wa Madaktari Bingwa hapa umesaidia kuwakumbusha miongozo na maadili ya watumishi wa afya, kuwaonesha umuhimu wa kuzingatia hatua mbalimbali katika kuwahudumia wajawazito na watoto na kutokupuuzia dalili mbalimbali zinazoonekana kwa wagonjwa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Translate »